Featured

    Featured Posts

GAVU AWATAKA WANACCM KUHUDHURIA VIKAO NA KULIPIA KODI

 


Katibu wa Nec Oganaizesheni  wa Chama cha Mapinduzi Issa haji Gavu amewataka wanachama wa CCM kuhudhuria vikao sambamba na kulipia kadi ili waendelee kuwa wanachama hai. 


Gavu amesema hayo Mei 29,2023 alipokuwa akizungumza na wananchi baada ya kushiriki Mkutano Kwa Balozi wa Shina Na. 04  Kata ya Ifunda katika halmashauri ya wilaya ya Iringa akiwa ameambatana na Katibu Mkuu wa CCM ambaye yupo mkoani Iringa kwa ziara ya siku 7 ya kukagua uhai wa chama na utekelezaji wa Ilani ya uchaguzi ya CCM. 


Amesema kuwa wanachama hai itasaidia CCM kuendelea kuwa chenye mvuto na oitaendelea kuaminiwa na kuthaminiwa na watanzania huku akisema hakuna chama chenye mvuto kwa wananchi  kama  CCM.


Katika hatua nyingine GAVU amesema Tanzania ni nchi yenye demokrasia ndio maana kumekuwa na majadiliano sambamba na kumpa Uhuru kila mtanzania kutoa maoni.



author

Author Name

Author Description!

Get Free Email Updates to your Inbox!

Post a Comment

www.CodeNirvana.in

Magazeti Ya Leo

Copyright © Magazeti ya Leo, Habari Leo Tanzania, Mwananchi, Michuzi, mwanaspoti, nipashe, Udaku | Designed By Code Nirvana