Featured

    Featured Posts

NDEREMO, SHANGWE VILITAWALA ZIARA YA KOMREDI CHONGOLO IRINGA

 

Shamra shamra na nderemo vilitawala wakati wa ziara ya siku 7 ya Katibu Mkuu wa CCM, Komredi Daniel Chongolo mkoani Iringa.

Mambo yaliyoibua furaha hiyo ni kazi kubwa aliyokuwa akiifanya ya kuwatenbelea viongozi wa mashina na kushiriki nao vikao, lakini kubwa zaidi ni kusikiliza kero zao na kuzitatua.

Kero kubwa alizozipatia ufumbuzi ni miundombinu ya barabara, afya, miradi ya maji, elimu, kilimo cha umwagiliaji, mawasiliano na hasa uwekaji wa minara na marambo ya kunyweshea mifugo.

Katika ziara hiyo yenye mafanikio makubwa  ambayo aliambatana na Katibu wa NEC Oganaizesheni, Issa Haji Gavu na Katibu wa NEC Itikadi na Uenezi, Sophia Mjema ilihitimishwa kwa mkutano mkubwa wa hadhara uliofanyika kwenye Uwanja wa Mwembetogwa mjini Iringa Juni Mosi, 2023.
Baadhi ya wananchi wakishangilia  baada ya Chongolo kuzindua upandaji wa samaki katika bwawa la Masaka katika Kata ya Kaning'ombe, Iringa Vijijini.
Mmoja wa wanachama wa CCM akishangilia wakati Chongolo akitatua baadhi changamoto aliposhiriki kikao cha shina namba 4 linaloongozwa na Mwenyekiti Deodata  Msasa katika Kijiji cha Bandamichi Ifunda..
Mbunge wa Kalenga, Jackson Kiswaga akiungana na wananchi kufurahi baada ya Komredi Chongolo kuahidi kutatua kero katika eneo la Bandamichi Ifunda ambapo aliagiza TAMISEMI kuhakikisha inapeleka haraka watumishi na vvifaa katika zahanati ambayo ujenzi wake umekamilika. Pia aliahidi katika Halmashauri ya Iringa kuwapatia magari mawili ya kubebea wagonjwa na moja la uangalizi.

Komredi Chongolo akielekea kwenye kikao cha shina namba 4 linaloongozwa na Mwenyekiti Deodata Msasa Kijiji cha Bandamichi, Ifunda.



Mambo yalivyokuwa wakati Chongolo alipokuwa akihutubia baada ya kukagua vibanda 16  vya biashara pamoja na mnara wa Vodacom eneo la Nyororo Jimbo la Mufindi Kusini Mei 28, 2023. 
Nderemo ziliibuka Chongolo akihutubia baada ya kukagua ujenzi wa Shule ya Sekondari Mufindi






PICHA ZOTE NA RICHARD MWAIKENDA
author

Author Name

Author Description!

Get Free Email Updates to your Inbox!

Post a Comment

www.CodeNirvana.in

Magazeti Ya Leo

Copyright © Magazeti ya Leo, Habari Leo Tanzania, Mwananchi, Michuzi, mwanaspoti, nipashe, Udaku | Designed By Code Nirvana