Featured

    Featured Posts

SURA MAKINI ZA JAMII YA KIMASAI WAKIMSIKILIZA KIONGOZI MAKINI CHONGOLO

Wananchi wa jamii ya kimasai wakimsikiliza kwa makini Katibu Mkuu wa CCM, Daniel Chongolo alipokuwa akihutubia katika mkutano wa Shina namba 7 katika Kijiji cha wafugaji cha  Mtandika, Ruaha Mbuyuni Mei 31, 2023 ambapo alisikiliza kero zao na kuzitafutia ufumbuzi.

Komredi Chongolo ambaye alikuwa kwenye ziara ya siku 7 ya kuhamasisha uhai wa CCM kuanzia ngazi ya shina, kukagaua utekelezaji wa Ilani ya Uchaguzi ya CCM na kusikiliza kero za wananchi katika kijiji hicho aliahidi  ujenzi wa vyumba sita vya madarasa ya shule ya msingi, kujenga rambo ya kunyweshea mifugo, kuwapelekea umeme na  mradi wa maji.

Katika ziara hiyoyenye mafanikio makubwa  ambayo aliambatana na Katibu wa NEC Oganaizesheni, Issa Haji Gavu na Katibu wa NEC Itikadi na Uenezi Sophia Mjema ilihitimishwa kwa mkutano mkubwa wa hadhara uliofanyika kwenye Uwanja wa Mwembetogwa mjini Iringa Juni Mosi, 2023.



Katibu Mkuu wa CCM, Komredi Chongolo akihutubia.














PICHA ZOTE NA RICHARD MWAIKENDA



 
author

Author Name

Author Description!

Get Free Email Updates to your Inbox!

Post a Comment

www.CodeNirvana.in

Magazeti Ya Leo

Copyright © Magazeti ya Leo, Habari Leo Tanzania, Mwananchi, Michuzi, mwanaspoti, nipashe, Udaku | Designed By Code Nirvana