Featured

    Featured Posts

WAZIRI AIPA TANESCO SIKU 5 TATIZO LA UMEME DAR

Waziri wa Nishati,  Dk Medard Kalemani ametoa siku tano kwa Shirika la Umeme Tanzania (Tanesco) kumaliza changamoto ya umeme kwenye maeneo yanayokosa nishati hiyo jijini Dar es Salaam.


Waziri huyo ameeleza kuwa hana taarifa za kuwepo kwa mgao wa umeme, hivyo ametoa muda huo endapo kuna dosari zozote zitafutiwe ufunguzi.


Ametoa agizo hilo leo Jumatano Februari 13, 2019 alipotembelea kituo cha kufua umeme cha Kurasini kukagua utekelezaji wa mradi wa kuboresha huduma ya umeme jijini Dar es Salaam.


Dk Kalemani ameeleza kuwa kuna ziada ya umeme zaidi ya megawati 260, atashangazwa na taarifa kuwa umeme unakosekana.

author

Author Name

Author Description!

Get Free Email Updates to your Inbox!

Post a Comment

www.CodeNirvana.in

Magazeti Ya Leo

Copyright © Magazeti ya Leo, Habari Leo Tanzania, Mwananchi, Michuzi, mwanaspoti, nipashe, Udaku | Designed By Code Nirvana