Katibu wa NEC Idara ya Organaizesheni Ndg. Issa Gavu amekutana na Baraza la wazee Mkoa wa Manyara na kufanya kikao cha pamoja 18 Nov 2023 Mkoani Manyara.
Katika kikao hicho wazee wamepata nafasi nzuri ya kutoa Maoni yao na ushauri kwa kwa Chama Cha Mapinduzi,ikiwa lengo ni Kukiimarisha, kukiendeleza na kukivusha Chama Cha Mapinduzi.
Aidha Ndg. Gavu amepata nafasi nzuri ya kushauriana na kujadiliana namna nzuri ya kukiimarisha Chama Cha Mapinduzi katika Ngazi zote hasa kipindi hiki cha Uchaguzi 2024 na 2025.
Pamoja na mambomengine Ndg. Gavu amepokea Salaam nyingi pamoja na Pongezi za Mwenyekiti wa CCM Ndg. Dkt.Samia Suluhu Hassan kutoka kwa wazee wa Mkoa wa Manyara kwa kutambua Umuhimu wa Mabaraza ya wazee Nchi nzima na kuanza na Mkoa wa Manyara.
Ndg. Issa Gavu amemaliza kwa kuwapongeza Wazee kwa mchango mzuri na Hekima pamoja na busara wanazotumia katika kukishauri Chama Cha Mapinduzi
”Hekima, Busara, Ushauri na uzoefu wenu Baraza la wazee katika mikoa yote Nchini ndani ya Chama Cha Mapinduzi ndiyo inayotofautisha Chama Cha Mapinduzi na vyama Vingine na hii ndiyo maana ya kauli mbiu ya wazee Isiyo Kongwe Haivushi” Amesema Ndg Gavu
#kaziIendelee
#isiyokongweHaivushi



Post a Comment