Shambulio hilo la maroketi na jibu la Israel havikusababisha madhara yoyote, kwa mujibu wa jeshi la Israel na watu mashuhuda katika eneo la Gaza.
Vijana wa Kipalestina wakikimbia mabomu ya kutoa machozi ya jeshi la Israel katika mpaka wa Gaza na Israel
Vifaru vya jeshi la Israel vilishambulia maeneo ya Hamas katikati ya ukanda wa Gaza na mashariki mwa mji wa Gaza, mashuhuda wamesema.
Mamia kwa maelfu ya wakaazi wa Gaza walijikusanya hapo mapema katika mpaka na Israel kukumbuka mwaka mmoja tangu maandamano na makabiliano kuzuka katika eneo hilo, lakini hofu ya mauaji makubwa yaliepukwa baada ya majadiliano yaliyoongozwa na Misri hapo kabla.
Wapalestina wanne waliuwawa na risasi kutoka jeshi la Israel , mmoja wakati wa maandamano kabla ya mkutano mkuu na wengine watatu vijana wa umri wa miaka 17 katika makabiliano jioni ya Jumamosi, wizara ya afya katika mji wa Gaza imesema. Wakaazi wengine 316 wa Gaza walijeruhiwa.
Mamia ya waandamanaji wa Kipalestina katika uzio wa mpaka kati ya Gaza na Israel
Lakini hofu ya kurejewa kwa maandamano kama hayo na makabiliano kwa wale walioshuhudia zaidi ya Wapalestina 60 waliuwawa hapo Mei 14, wakati Marekani ilipohamisha ubalozi wake nchini Israel kwenda Jerusalem, hayakutokea.
Israel iliweka maelfu kadhaa ya wanajeshi katika mpaka, wakati kumbukumbu hiyo ikija katika wakati nyeti kabla ya uchaguzi wa hapo Aprili 9.
Upatanishi wa Misri
Misri imejaribu kufanya upatanishi kati ya Israel na watawala wa eneo la Gaza kundi la mrengo wa Kiislamu la Hamas kuzuwia ghasia.
Maafisa wa Hamas wanasema makubaliano yamefikiwa ambayo yatashuhudia Israel ikilegeza mzingiro wake unaoathiri eneo la Gaza , kwa kupata hali ya utulivu wa maandamano
Mamia kwa maelfu ya walijikusanya katika maeneo matano katika mpaka huo lakini wengi wa watu walibakia mbali na uzio wa mpaka.
Kijana wa Kipalestina akiwa na ujumbe kwa Israel kuondoa mzingiro wa muongo mmoja sasa katika eneo hilo
Mashariki mwa mji wa Gaza, makundi madogo ya vijana wanaume walikaribia uzio na kutaka kuuvunja mara kadhaa lakini walilazimishwa kurejea nyuma na mabomu ya kutoa machozi ya vikosi vya Israel.
Waandamanaji walirusha mawe dhidi ya wanajeshi wa Israel.
Ujumbe wa usalama kutoka Misri ulifanya ziara katika maeneo ya maandamano katika mji wa Gaza, kama walivyofanya viongozi wa Hamas Ismail Haniya na Yahya Sinwar.
Jeshi la Israel lilisema karibu "wafanya ghasia na waandamanaji" 40,000 walikusanyika katika maeneo mbali mbali katika mpaka huo.
Jeshi hilo lilisema maguruneti na viripuzi vilirushwa dhidi ya wanajeshi hao, ambao nao walijibu "kwa mujibu wa viwango vya utaratibu wao wa kufanya kazi".
Vijana wa Kilaestina wakirusha viripuzi kutoka upande wa Gaza
Waandamanji walikuwa wakikumbuka mwaka mmoja wa wiki ya maandamano ya ghasia ya kila mara ambamo kiasi ya Wapalestina 200 na mwanajeshi mmoja wa Israel waliuwawa.
Takriban watoto 50 wa Kipalestina waliuwawa katika ukanda wa gaza tangu maandamano hayo kuanza, kundi la hisani la Save The Children limesema.
Post a Comment