Featured

    Featured Posts

NSIMA AZINDUA KWA KISHINDO MAADHIMISHO YA WIKI YA WAZAZI KITAIFA MKOANI RUKWA, LEO

Katibu Mkuu wa Jumuiya ya CCM ya Umoja wa Wazazi Tanzani Erasto Sima akishiriki kupanga matofali ya ujenzi wa hosputali ya Nkasi, katika mji mdogo wa Namanyere mkoani Rukwa, ikiwa ni sehemu ya uzinduzi wa Wiki ya Jumuiya hiyo Kitaifa, leo.

Na Bashir Nkoromo, Nkasi
Katibu Mkuu wa Jumuiya ya Chama Cha Mapinduzi ya Umoja wa Wazazi Tanzani, Erasto Sima leo amezindua kwa kishindo Maadhimisho ya Wiki ya Jumuiya hiyo Kitaifa katika mji mdogo wa Namanyere wilayani Nkasi mkoani Rukwa.

Uzinduzi huo ameufanya kwa mkutano maalum uliohudhuriwa na viongozi mbali mbali wa Jumuiya zote CCM ukitanguliwa na shuguli ya kukagua Zahanati ya Nyamanyere na ujenzi wa Hosoitali ya Wilaya ya Nkasi.

Manaibu Katibu Mkuu wa Jumuiya hiyo Tija Magoma (Bara) na Othman Ali Maulid (Zanzibar) ni miongoni mwa viongozi walioshiki kwa karibu shughuli mbalimbali za uzinduzi wa maadhimisho hayo pamoja na viogozi wa Jumuiya zote za CCM tangu ngazi ya mkoa huo wa Rukwa.

Baada ya kuwasili Namanyere na ujumbe wake akitokea Mjini Sumbawanga, Nsima alizungumza na umati wa Wana CCM na viongozi mbalimbali katika viwanja vya Zahanati ya Namanyere ambako alikuta Kada wa CCM Mkuu wa Wilaya hiyo Saidi Mtanda akiongoza wana CCM hao na Wananchi kufanya kufanya usafi wa mazingira kwenye Zahanati hiyo.

Akizungumza. Nsima aliwataka wananchi kujenga tabia ya kupeleka watoto kwenye zahanati hiyo wanapougua badala ya kukaa nao nyumbani kwa kuwa serikali imeijenga na kuiboresha kwa kuwa inajali afya za wananchi.

Aliwataka pia kujitolea damu mara kwa mara ili kusawiri lengo la serikali kuweka benki ya damu kwenye zahanati hiyo, akisema ni lazima wajivunie kwa kufanya hivyo kwa sababu ni zahanati chache nchini ambazo zina huduma ya benki ya damu kama ilivyo ya Namanyere.

Sima aliwataka wananchi kuunga mkono juhudi za kuboresha maisha ya wananchi zinazofanywa na Serikali CCM ya awamu ya tano chini ya Rais Dk. John Magufuli ambapo Katibu Mkuu huyo wa Jumuiya ya Wazazi Tanzania alieleza miradi ya kimaendeleo na huduma zilizokwisha tekelezwa na zinazoendelea kutekelezwa chini ya uongozi wa Rais Dk. Magufuli.

Baadaye Nsima aliikagua zahanati hiyo na kushudia ilivyoboreshwa hasa upande wa majengo ikiwemo chumba cha kisasa cha kuhifadhia maiti ambapo alihitimisha ukaguzi huo kwa yeye na msafara wake kupanda miti ya aina mbalimbali.

Nsima alimaliza ziara kwa kukagua ujenzi wa hopsitali kubwa ya Wilaya ya Namanyere ambayo itakuwa na uwezo wa kuhudumia wakazi wa wilaya hiyo na wa maeleneo ya wilaya jirani ambako alishiriki kupanga matofali yanayofyatulia hapo kwa ajili ya ujenzi huo.

Akizungumza na viongozi kwenye mkutano wa ndani wa kuzindua maadhimisho hayo, Nsima aliwataka wananchi kuwafichua watendaji au viongozi watakaokuwa wanazembea kushiriki kikamilifu utekelezaji wa ilani ya CCM.

Nsima ataendelea kuwepo mkoani Rukwa akishirikiana na wananchi kufanya shughuli mbalimbali za kijamii katika wilaya tofauti tofaiti za mkoa huo hadi Aprili 6, 2019, kabla ya jerejea mjini Sumbawanga ambako Mwenyekiti wa Jumuiya ya Wazazi Tanzania Dk. Edmund Mndolwa atafunga kilele cha maadhimisho hayo kesho yake.

author

Author Name

Author Description!

Get Free Email Updates to your Inbox!

Post a Comment

www.CodeNirvana.in

Magazeti Ya Leo

Copyright © Magazeti ya Leo, Habari Leo Tanzania, Mwananchi, Michuzi, mwanaspoti, nipashe, Udaku | Designed By Code Nirvana