Featured

    Featured Posts

MTEMVU FOUNDATION YATOA MSAADA WA VYAKULA KWENYE MAKUNDI MAALUMU

Mwenyekiti wa Mtemvu Foundationi na aliyewahi kuwa Mbunge wa Jimbo la Temeke, Abbas Mtemvu akizungumza na waandishi wa habari ofisini kwake Jijini Dar es Salaam  alisema; Tukiendeleza Desturi yetu karibu mwaka wa 17 kutoa vitu kama hivi vyakula na vitu mbalimbali kwa makundi ya yatima, makundi ya wajane, makundi ya wasio jiweza, wenzetu walemavu na kadhalika.

Kwahiyo mwendelezo huu ni wakila mwaka na tutaendelea kutoa kadiri Mungu atakavyotujalia afya na nitoe wito wangu ambao ni uleule wa kila siku kwamba kutoa ni moyo na tujitahidi kila mtu ukiwa na kidogo toa na hata ukiwa na nguo 10 au 20 najuwa huvai zote unaweza kutoa nguo mbili tatu kusaidia nduguzetu watanzania najuwa watanzania ni wakarimu tuendelee kusaidia wasio jiweza katika mwezi wa Ramadhani na miezi mingine yote ambapo na mama Mtemvu alisema;

Nianze kwa kumshukuru Mungu kwa kutuwezesha kufanikisha azma yetu ya kila mwaka mara ifikapo mwezi Mtukufu wa Ramadhani ambapo sasa miaka 17 mfululizo

Hutoa tulicho jaaliwa katika vitu mbalimbali kwa watoto yatima, walemavu na makundi mengine yote tunayo hapa, kutoa hivi sikama vitatosheleza lakini angalau wanafarijika na wanaona kunawatu wanao wakumbuka, wito wangu ni kwamba wadau wengine wajitokeze kuwasaidia wenzetu hawa


    Aliyekuwa Mbunge wa Jimbo la Temeke, Abbas Mtemvu akimkabidhi Jasmin John kutoka kundi maalumu la Kinamama wenye ulemavu msaada kwa ajili ya kundi hilo.








author

Author Name

Author Description!

Get Free Email Updates to your Inbox!

Post a Comment

www.CodeNirvana.in

Magazeti Ya Leo

Copyright © Magazeti ya Leo, Habari Leo Tanzania, Mwananchi, Michuzi, mwanaspoti, nipashe, Udaku | Designed By Code Nirvana