Featured

    Featured Posts

RAIS DK. MAFUFULI AONDOKA NCHINI LEO KWENDA AFRIKA KUSINI

Rais Dk. John Magufuli
akiagana na Mkuu wa Majeshi Jenerali Venance Mabeyo wakati akiondoka
katika Uwanja wa Ndege wa Kimataifa wa Julius Nyerere  kuelekea Afrika
ya Kusini leo asubuhi, ambapo kesho atahudhuria sherehe za kuapishwa
kwa Rais wa nchi hiyo Cyril Ramaphosa mjini Pretoria
Ikulu, Dar es Salaam
Rais Dk. John Magufuli leo Mei 24, 2019 ameondoka nchini kwenda Afrika ya Kusini kuhudhuria sherehe za kuapishwa kwa Rais Mteule wa nchi hiyo, Cyril Ramaphosa, itakayofanyika kesho.

Katika safari hiyo Rais Magufuli ameongozana na Rais Mstaafu Dk. Jakaya Kikwete, Makamu Mwenyekiti wa Chama Cha Mapinduzi (CCM) Mzee Philip Mangula na Waziri wa Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Afrika Mashariki, Prof. Palamagamba Kabudi.

Wakizungumza kabla ya kuondoka, Rais Mstaafu Kikwete na Makamu Mwenyekiti wa CCM Mzee Mangula wamesema Tanzania na Afrika ya Kusini zina uhusiano mkubwa na wa kihistoria na kwamba Serikali na chama zina kila sababu ya kudumisha uhusiano na ushirikiano huo.

Viongozi hao wameondoka katika Uwanja wa Ndege wa Kimataifa wa Julius Nyerere Jijini Dar es Salaam, kwa kutumia ndege ya Shirika la Ndege Tanzania (ATCL).

Waziri wa Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Afrika Mashariki, Prof. Palamagamba Kabudi amesema baada ya kuhudhuria sherehe za kuapishwa kwa Rais Mteule wa Afrika ya Kusini, Rais Magufuli atafanya ziara Rasmi ya Kitaifa nchini Namibia ambako pia atazindua mtaa uliopewa jina la Baba wa Taifa Hayati Mwalimu Julius Kambarage Nyerere kwa kutambua mchango mkubwa alioutoa katika ukombozi wa Taifa hilo.
author

Author Name

Author Description!

Get Free Email Updates to your Inbox!

Post a Comment

www.CodeNirvana.in

Magazeti Ya Leo

Copyright © Magazeti ya Leo, Habari Leo Tanzania, Mwananchi, Michuzi, mwanaspoti, nipashe, Udaku | Designed By Code Nirvana