Featured

    Featured Posts

MKUCHIKA AFUNGUA MAFUNZO YA MFUMO MPYA WA “AJIRA PORTAL” KWA MAAFISA WA SERIKALI.

Baadhi ya washiriki wa mafunzo ya mfumo mpya wa “Ajira Portal” wakimsikiliza Waziri wa Nchi, Ofisi ya Rais, Menejimenti ya Utumishi wa Umma na Utawala Bora, George Mkuchika  (hayupo pichani) wakati wa ufunguzi wa mafunzo hayo yaliyofanyika  jijini Dodoma.

Waziri wa Nchi, Ofisi ya Rais, Menejimenti ya Utumishi wa Umma na Utawala Bora, George Mkuchika (akifungua mafunzo ya mfumo mpya wa “Ajira Portal” kwa Maafisa Rasilimaliwatu serikalini yaliyofanyika  jijini Dodoma.



Katibu wa Sekretarieti ya Ajira katika Utumishi wa Umma, Xavier Daudi  akifafanua changamoto za mifumo ya awali ya uombaji kazi, kabla ya ufunguzi wa mafunzo ya mfumo mpya wa “Ajira Portal” kwa Maafisa Rasilimaliwatu jijini Dodoma.

Mkurugenzi wa Idara ya Usimamizi Rasilimaliwatu, Ofisi ya Rais, Menejimenti ya Utumishi wa Umma na Utawala Bora, ACP Ibrahim Mahumi akizungumza kabla ya ufunguzi wa mafunzo ya mfumo mpya wa “Ajira Portal” kwa Maafisa Rasilimaliwatu jijini Dodoma.

Mkuchika akiwa katika picha ya pamoja na  baadhi ya Wakurugenzi na Wakurugenzi Wasaidizi wa  serikali baada ya kufungua mafunzo ya mfumo mpya wa “Ajira Portal” kwa Maafisa Rasilimaliwatu jijini Dodoma.  Wengine ni Katibu wa Sekretarieti ya Ajira katika Utumishi wa Umma, Xavier Daudi  (kulia) na Mkurugenzi wa Idara ya Usimamizi Rasilimaliwatu, Ofisi ya Rais, Menejimenti ya Utumishi wa Umma na Utawala Bora, ACP Ibrahim Mahumi (kushoto).

author

Author Name

Author Description!

Get Free Email Updates to your Inbox!

Post a Comment

www.CodeNirvana.in

Magazeti Ya Leo

Copyright © Magazeti ya Leo, Habari Leo Tanzania, Mwananchi, Michuzi, mwanaspoti, nipashe, Udaku | Designed By Code Nirvana