Bunge la Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Leo Sept.3,2019 limefanya azimio la kumpongeza Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dokta John Pombe Magufuli baada ya hivi Karibuni kupewa nafasi ya kuwa Mwenyekiti wa Bunge la Jumuiya Ya Madola Afrika SADC.
Mwenyekiti kamati ya Bunge ya Mambo ya nje na Usalama Mhe. Musa Azan Zungu amesema Waasisi wa Jumuiya ya maendeleo nchi wanachama wa Kusini Mwa Afrika wamefanya makubwa ikiwa ni pamoja na kuunganisha nchi wanachama hivyo matamanio ya waasisi hao ikiwa ni pamoja na Rais wa awamu ya Kwanza Mwl.Julius Kambarage Nyerere na Aman Abeid Karume yanatimizwa na Rais Magufuli katika kusukuma mbele maendeleo .
Nao baadhi ya Wabunge wamesema kuchaguliwa kwa Rais Magufuli kuwa Mwenyekiti wa SADC itasaidia kuondoa kuritimba wa masoko katika biashara huku pia wakisema kuwa Tanzania ni Kitovu cha Cha Ukombozi kwa nchi wanachama wa SADC katika kupigania Uhuru.
Akihitimisha katika Azimio hilo la Pongezi bungeni jijini Dodoma Mhe.Zungu amesema ili Nchi wanachama wa SADC kujikomboa lazima kwanza kutafuta masoko ya ndani
Post a Comment