Mamia ya wananchi wa Afrika Kusini wamekuwa wakionekana wakikimbia na kupora mali za watu tangu Jumapili katika eneo lenye shughuli za kibiashara na kuchoma moto maduka yanayoaminiwa kumilikiwa na wahamiaji kutoka mataifa ya Afrika.
Ghasia hizo zilianzia katika eneo la Jeppestown, lililopo katika wilaya ya kati yenye shughuli za biashara. Lakini zilisambaa hadi kwenye maeneo mengine kama vile Denver, Malvern, Turffontein, Tembisa na maeneo mengine ya vitongoji vya jiji la Johansburg.
Post a Comment