Featured

    Featured Posts

RAIA WA CHINA KIZIMBANI KWA KUINGIZA MIFUKO YA PLASTIKI


Na Karama Kenyunko, Blogu ya Jamii
WAFANYAKAZI wawili wa Shirika la Viwango Tanzania (TBS) na Mkurugenzi wa kiwanda cha Waadilifu ambae ni raia wa China wamefikishwa katika Mahakama ya Hakimu Mkazi Kisutu wakikabiliwa na mashtaka matano likiwemo la matumizi mabaya ya madaraka na kusaidiwa kuingizwa nchini kwa marobota ya mifuko Wa plastiki isiyokuwa na viwango  ya thamani ya  zaidi ya Sh Milioni 73.

Akisoma hati ya mashtaka wakili wa serikali, Janeth Magoho amewataja washtakiwa hao kuwa ni, Wasalim Msulamdunda na Aman Mollel ambao ni wafanyakazi wa TBS na Zoupa Michael, raia wa china.
 Imedaiwa mbele ya Hakimu Mkazi Victoria Mwaikambo kuwa,  siku na mahali pasipojulikana, washtakiwa wote kwa pamoja walikula njama ya kuingiza nchini mifuko ya plastiki isiyokuwa na viwango.

Katika shtaka la pili linalowakabili, Msulamdunda na Molle, imedaiwa, kati ya Agosti 2 na 6 2019 jijini Dar es Salaam, washtakiwa kwa kutumia nafasi yao kazini, waliongoza genge la uhalifu kwa kuruhusu uingizwaji wa marobota 255 ya mifuko ya plastiki hiyo nchini Tanzania yenye thamani ya sh. 73885531 ambayo haikuwa imeidhinishwa na TBS.

Pia  mshtakiwa Michael anadaiwa kuwa siku na mahali hapo, akiwa siyo mtumishi wa umma (TBS) kwa kushirikiana na watumishi hao wa TBS  kwa makusudi waliingiza mali kwenye masoko ambayo ni mifuko hiyo ya plastiki kinyume na sheria ya nchi.

Katika shtaka la nne imedaiwa, Agosti 17, mwaka huu huko eneo la Mbezi Makonde mshtakiwa Michael alikutwa na wakaguzi wa Baraza la Taifa la Uhifadhi na Usimamizi wa mazingira (NEMC) pamoja na mkaguzi wa TBS  wakiingiza nchini mifuko hiyo ya plastiki kutoka China  ambayo haijaidhinishwa na TBS.

Pia washtakiwa Msulamdunda na Molle, wanadaiwa kati ya Agosti 2 na 6, 2019  wakiwa waajiriwa wa TBS kama maafisa wa Viwango na wakaguzi walitumia madaraka yao vibaya kwa kushindwa uwahibika na kutimiza majukumu yao kwa kusababisha na kuruhusu kuingizwa nchini kwa mifuko hiyo ya plastiki isiyokuwa na viwango ambayo haijaidhinishwa TBS.

Hata hivyo, washtakiwa wamekana shtaka hilo na wamerudishwa rumande kwa kuwa Mahakama ya Hakimu Mkazi Kisutu, haina mamlaka ya kusikiliza kesi za uhujumu uchumi wala kutoa dhamana hadi Mahakama Kuu.

Kesi hiyo imeahirishwa hadi Septemba 17, washtakiwa wote wamerudushwa rumande.
author

Author Name

Author Description!

Get Free Email Updates to your Inbox!

Post a Comment

www.CodeNirvana.in

Magazeti Ya Leo

Copyright © Magazeti ya Leo, Habari Leo Tanzania, Mwananchi, Michuzi, mwanaspoti, nipashe, Udaku | Designed By Code Nirvana