Rais wa Uturuki Recep Tayyip Erdoğan, amempokea makamu waziri mkuu wa Qatar ambaye pia ni waziri wa mambo ya nje wa nchi hio Sheikh Muhammed bin Abdurrahman bin Casim El Sani.Wawili hao walifanya mkutano wa ndani ambao haukuruhusiwa wanahabari, mkutano huo ulifanyika kwenye kasri la Huber lililopo Tarabya Istanbul na ulidumu kwa muda wa saa 1 na dk 25.
Mkutano huo ulihudhuriwa pia na waziri wa hazina na uchumi wa Uturuki, Berat Albayrak na waziri wa mambo ya nje wa Uturuki, Mevlüt Çavuşoğlu.
Post a Comment