Featured

    Featured Posts

MAHAFALI YA PILI YA KUMALIZA ELIMU YA MSINGI MISITU YAFANA DAR




Walimu wakiwa wamembeba mwanafunzi bora wa nidhamu, Mara Mwita baada ya kutangazwa katika sherehe za Mahafali ya Pili ya kumaliza Elimu ya Msingi katika Shule ya Msingi Misitu, Kivule, wilayani Ilala, Dar es Salaam jana. Wanafunzi 182 walihitimu. PICHA ZOTE NA RICHARD MWAIKENDA


Wanafunzi wakicheza ngoma wakati wa sherehe hizo za mahafali kwenye viwanja vya shule hiyo.


Wanafunzi wakicheza shoo ya muziki wa kihindi wakati wa kuwaaga wanafunzi waliomaliza darasa la saba  katika Shule ya Msingi Misitu, Kivule, Dar es Salaam.


 Wanafunzi waliokuwa wanaagwa wakiimba wimbo wakati wa mahafali hayo.





Baadhi ya wazazi wakiwa katika sherehe za mahafali yao.


 Mkurugenzi wa Shule ya Msingi Zawadi na Sekondari ya Zawadi, Joseph Mofati, ambaye alikuwa mgeni rasmi katika mahafali hayo, akihutubia na kuhamasisha wananchi kuchangia fedha za kusaidia kufanikisha ujenzi wa matundu ya vyoo vya shule, ofisi ya Mwalimu Mkuu na Ofisi ya Waalimu wa shule ya Msingi Misitu. Mofati alichangia mifuko 50 ya saruji. Kushoto kwake ni Diwani wa Kata ya Kivule, Mollel Amos.
 Mwanafunzi  aliyemaliza darasa la saba, Fatuma Nassoro akipokea cheti kutoka kwa Mgeni rasmi, Joseph Mofati wakati wa mahafali hayo.

Mwalimu Mkuu wa Shule ya Msingi Misitu, Yasinta Hugo akihamasisha wananchi kuchangia fedha za kusaidia kufanikisha ujenzi wa matundu ya vyoo vya shule, ofisi ya Mwalimu Mkuu na Ofisi ya Waalimu wa shule ya Msingi Misitu. 
author

Author Name

Author Description!

Get Free Email Updates to your Inbox!

Post a Comment

www.CodeNirvana.in

Magazeti Ya Leo

Copyright © Magazeti ya Leo, Habari Leo Tanzania, Mwananchi, Michuzi, mwanaspoti, nipashe, Udaku | Designed By Code Nirvana