Mkurugenzi Mkuu wa zamani wa Idara ya Usalama wa Taifa (TISS), Apson Mwang'onda amefariki Dunia akiwa nchini Afrika Kusini alikokuwa akipatiwa matibabu.
Awali alilazwa katika Hospitali ya Taifa Muhimbili jijini Dar es Salaam akiungua saratani na baadaye kuhamishiwa nchini Afrika Kusini ambako mauti yamemkuta na mwili wake unatarajiwa kuletwa nchini kesho au keshokutwa.
Mwang'onda aliongoza Idara ya usalama wa taifa katika Kipindi cha Awamu ya tatu ya Urais chini ya Benjamin Mkapa katika ya mwaka 1995 na 2005 na baadaye kumwachia nafasi hiyo Othamn Rashid.
Post a Comment