Featured

    Featured Posts

MKURUGENZI MTENDAJI BENKI YA CRDB AWAHAMASISHA WAZAZI KUWAFUNGULIA WATOTO AKAUNTI


Mkurugenzi Mtendaji wa Benki ya CRDB, Abdulmajid Nsekela (wa pili kulia) akimkabidhi cheti Mwanafunzi wa Shule ya Sekondari ya Helasita, Ibrahim Sylvester Tati ambaye amekuwa kinara katika masomo, wakati wa mahafali ya kwanza ya Shule hiyo, iliyopo Kijichi jijini Dar es salaam. Kulia ni Mwenyekiti wa Bodi ya Shule hiyo, Amulyke Ngeliama akifuatia na Mkurugenzi Mkuu wa Shule ya Sekondari Helasita, Joseph Sanga

Mkurugenzi Mtendaji wa Benki ya CRDB, Abdulmajid Nsekela amewahamasisha wazazi kuwafungulia watoto wao akaunti kwani husaidia kuwajengea uelewa juu ya masuala ya fedha. Nsekela ameeleza hayo wakati wa mahafali ya kidato cha nne katika shule ya Sekondari Helasita yaliyofanyika wikiendi hii.

Nsekela alisema wazazi wanapaswa kuelewa kuwa pamoja na elimu ambayo watoto wanaipata shule, wanatakiwa kupata elimu na uelewa juu ya masuala ya fedha hususani katika kujiwekea akiba. 

“Hii itawasaidia watoto kujijengea uwezo mkubwa katika masuala ya fedha na kujua namna bora ya kutimiza malengo yake,” alisema Nsekela.
Mkurugenzi Mtendaji wa Benki ya CRDB, Abdulmajid Nsekela akipata maelezo ya mfumo wa binadamu kutoka kwa Mwanafunzi wa kidato cha pili wa Shule ya Sekondari Helasita, Andebwise Mwambaya, wakati alipotembelea kazi mbalimbali zinazofanywa na wanafunzi hao, wakati wa mahafali ya kwanza ya Shule hiyo, iliyopo Kijichi jijini Dar es salaam mwishoni mwa wiki.

Nsekela alisema Benki ya CRDB kupitia kauli mbiu yake ya Ulipo Tupo imefanikiwa kubuni akaunti maalum kwa ajili ya watoto yaani “Junior Jumbo” na “Teens Account” pamoja na akaunti ya “Scholar” maalum kwa ajili ya wanafunzi wa elimu ya juu. “Ni wahakikishie tu, Benki ya CRDB ipo Tayari kuwahudumia,” aliongezea Nsekela.

Akitoa hotuba yake katika mahafali hayo, Nsekela aliupongeza uongozi wa shule ya sekondari Helasita kwa kuweza kuwajenga wanafunzi katika maadili mema na kuifanya shule hiyo kuwa kinara katika masomo katika wilaya ya temeke.
Mkurugenzi Mtendaji wa Benki ya CRDB, Abdulmajid Nsekela akipata maelezo ya mfumo wa kompyuta kutoka kwa wafunzi.

Nsekela pia aliwaasa wanafunzi wanaohitimu kuendelea kusoma kwa badii ili kuweza kufanya vizuri katika mitihani yao ya mwisho. “Napenda kuwakumbusha vijana wetu mnaohitimu leo kuwa bado safari yenu kimasomo inaendelea kwani tunaimani ya kuwa wote mtafaulu katika daraja la kwanza na kujiunga na kidato cha tano,” alisema Nsekela.

Nsekela alihitimisha kwa kusema kuwa vijana wanapaswa kufahamu kuwa wao ndio wamebeba mstakabali wa Taifa la Tanzania, kwani taifa lina nafasi ya kuwa endelevu likipata watendaji walio na viwango bora.
Mkurugenzi Mtendaji wa Benki ya CRDB, Abdulmajid Nsekela akiteta jambo na Mkurugenzi Mkuu wa Shule ya Sekondari Helasita, Joseph Sanga wakati wa mahafali ya kwanza ya Shule hiyo, iliyopo Kijichi jijini Dar es salaam mwishoni mwa wiki.
Mkurugenzi Mtendaji wa Benki ya CRDB, Abdulmajid Nsekela ambaye alikuwa mgeni rasmi kwenye mahafali ya kwanza ya Shule ya Sekondari ya Helasita, iliyipo Kijichi jijini Dar es salaam, akipata maelezo kutoka kwa Mwalimu Neema Machali, kupitia mchoro wa shule hiyo.
Picha ya pamoja.
author

Author Name

Author Description!

Get Free Email Updates to your Inbox!

Post a Comment

www.CodeNirvana.in

Magazeti Ya Leo

Copyright © Magazeti ya Leo, Habari Leo Tanzania, Mwananchi, Michuzi, mwanaspoti, nipashe, Udaku | Designed By Code Nirvana