Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. John Pombe Magufuli akizungumza na wananchi Mbozi katika mkutano uliofanyika katika mji wa Vwawa mkoani Songwe.
Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. John Pombe Magufuli akiwasalimia wakazi wa Mbozi wakati akitoka kuweka jiwe la msingi mradi wa uboreshaji wa huduma ya maji Vwawa mkoani Songwe.
Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. John Pombe Magufuli akiangalia vikundi vya ngoma za asili kabla ya kuwahutubia wananchi wa Vwawa mkoani Songwe.
Wananchi wa Mbozi wakifurahia hotuba ya Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. John Pombe Magufuli wakati akiwahutubia katika mji wa Vwawa.
Waziri wa Kilimo Japhet Hasunga akicheza ngoma ya kiasili wakati kikundi cha Vwawa kikitumbuiza mara baada ya Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. John Pombe Magufuli kuwasili katika eneo hilo.
Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. John Pombe Magufuli akisalimiana na Mbunge wa Momba (Chadema) David Silinde mara baada ya kuwahutubia wananchi Mbozi katika mkutano uliofanyika katika mji wa Vwawa mkoani Songwe. PICHA NA IKULU
Post a Comment