Featured

    Featured Posts

RC MAKONDA AZINDUA MFUMO WA KUWEZESHA WANANCHI KUTOA MALALAMIKO DHIDI YA WATENDAJI WASIOTEKELEZA MAJUKUMU YAO KWA KUTUMIA SIMU ZA MKONONI.


 
Mkuu wa Mkoa wa Dar es salaam Mhe. Paul Makonda leo October 09 amezindua Mfumo wa kuwawezesha wananchi wa Mkoa huo kuwasilisha kero na changamoto walizonazo kwa kutumia simu ya mkononi au Computer na ujumbe wao kuwafikia watendaji kwa haraka na kupatiwa majibu ndani ya muda mfupi jambo litakalosaidia kuokoa Muda na gharama za usafiri.

RC Makonda amesema ameamua kuanzisha mfumo huo baada ya kubaini kuwa wananchi wengi wamekuwa wakifika kwenye ofisi za umma na kupewa majibu ya “Njoo Kesho” pasipokujua kuwa wamepoteza muda na nauli zao kufuata huduma.

Aidha RC Makonda amebainisha kuwa mfumo huo utakuwa ukipokea taarifa za malalamiko ya Watendaji wasiowajibika kuanzia ngazi ya Mtaa, Kata, Wilaya hadi Mkoa na taarifa zitawafikia Viongozi wote kuanzia RC Makonda mwenyewe, Mkuu wa Wilaya husika, Mkurugenzi, Katibu tawala na Mkuu wa idara.

Hata RC Makonda amewahimiza wananchi kutumia mfumo huo kueleza kero zote zinazowakabili ikiwemo Afya, Barabara, Elimu, Maji, Umeme, Miradi inayokwama pamoja na kutoa taarifa pindi wanapobaini uhalifu kwenye mtaa.

Jinsi kuwasilisha ujumbe andika neno DSM kisha eleza changamoto zako kisha tuma kwenye namba 11000 au ingia kwenye Website https://ift.tt/2MnHjoa na ujumbe wako utapokelewa mara moja na kupewa mrejesho.
author

Author Name

Author Description!

Get Free Email Updates to your Inbox!

Post a Comment

www.CodeNirvana.in

Magazeti Ya Leo

Copyright © Magazeti ya Leo, Habari Leo Tanzania, Mwananchi, Michuzi, mwanaspoti, nipashe, Udaku | Designed By Code Nirvana