Mkuu wa mkoani Njombe Christopher Olesendeka
NJOMBE
Mkuu wa mkoa Njombe Christopher Olesendeka ametoa siku mbili kwa wadaiwa sugu waliosababisha kufilisika kwa benki ya wananchi Njombe NJOCOBA kujisalimisha wenyewe octoba 22 saa nne asubuhi katika ukumbi wa halmashauri ya wilaya ya Njombe ili kuweka maridhiano ya lini watazirejesha fedha hizo huku pia akitoa onyo kwa yeyote atakae puuza wito huo kukumba na nguvu ya vyombo vya dola.
Akizungumza katika kikao cha ushauri wa barabara RCC mkoa wa Njombe Christopher Olesendeka amesema Benki ya Njocoba ambayo ilikuwa tegemeo kubwa kwa wakazi mkoani humo haiwezi kufia mikononi mwake na kuwakosesha huduma wananchi hivyo ameanza msako wa watu waliohusika kuifilisi ili waweze kuweka makubaliano ya lini watarejesha fedha walikopeshana kienyeji na kwa kujuana bila kuzingatia taratibu.
Wakati akitangaza siku ya jumanne kukutana na wadaiwa sugu wa benki ya NJOCOBA, Olesendeka pia ametangaza octoba 24 kukutana na viongozi wa vyama vyote vya ushirika ambavyo vimekufa kutokana na utaratibu mbovu wa ukopeshaji fedha pamoja na matumizi mabovu ya fedha na kwamba kiongozi ambaye hataona umuhimu wa kufanya hivyo jeshi la polisi limkamate na kumtia mbaroni kwa masaa kadhaa.
Kwa upande wao wakazi wa mji wa Njombe akiwemo Odilo Mathias wanasema uamuzi uliochukuliwa na serikali ni uamuzi mzuri na wenye tija kwa wananchi kwa kuwa ilikuwa ikitoa huduma za pembejeo za kilimo, elimu ya fedha pamoja na kuweka na kukopa.
Aidha wamesema kufungwa kwake kumeathiri mzunguko kwa fedha kwa kuwa imefungwa na fedha nyingi za wateja wake.
Hatua hiyo inapokelewaje na wakazi wa mji wa Njombe , hapa ni baadhi yao akiwemo Odilo Mathias na Rozana ngimbuzi wanaeleza hisia zao.
Benki ya wananchi Njombe ilifungwa na BOT mwaka 2017 baada ya kubainika kuwa imeshindwa kujiendesha.
Post a Comment