CCM Blog, Dodoma
Katibu Mkuu wa CCM Dk. Bashiru Ally (pichani), ameziagiza Kamati za siasa za wilaya, Kata na Matawi kutowateuwa wagombea wenye sifa za hovyo ikiwemo kashfa za kuhujumu Ushirika, kuuza ardhi za wananchi na wenye mwenendo usioaminika kwenye jamii.
Taarifa ya Makao Mkuu ya CCM Dodoma, imesema agizo hilo amelitoa leo Oktoba 12, 2019, wakati akizungumza katika mkutano wa ndani wa wenyeviti wa mashina, viongozi wa CCM na serikali ngazi zote za Mkoa, wilaya, kata na matawi, katika Wilayani Liwale mkoani Lindi.
"Tukitaka kuzuia viongozi wababaishaji, Kangomba, Obutura, wadhulumaji wa ardhi, tuwe makini kwenye uchaguzi huu, kama kuna kiongozi aliwahi kuuza ardhi kwa kuwaibia wananchi, asiteuliwe na vikao vya CCM, na kama akihonga akapitishwa, wananchi msimchgue mtu huyo na sisi tutashughulika na waliomteua." Taarifa hiyo imemkari Dk. Bashiru akisema na kuongeza;
"CCM haiingii kwenye uchaguzi ili tu kushinda na kupata viongozi, ila inaingia ili ishinde na ipate viongozi bora watakao wahudumia wananchi, kwa kuwa imeahidi kuwatumikia wananchi kwa haki".
Katibu Mkuu amewataka wana-CCM watakao shindwa kwa namana yoyote kwenye kura za maoni kutosusa kwa hasira na kwenda vyama vingine kwa kwa sababu awamu hii Chama kitaweka nguvu zaidi eneo ambalo mwana CCM amehama na kwenda kugombea upinzani, hivyo, CCM itamshinda naye atakufa kisiasa.
Kwa mujibu wa taarifa hiyo, ameelekeza kuwa mwana-CCM yeyote atakayeshindwa kwenye kura za maoni kwa hujuma, atulie na kushirikiana na aliyeshinda, baada ya uchaguzi atasikilizwa na waliohusika na hujuma watawajibishwa kwa mujibu wa katiba na kanuni za Chama.
Pia Katibu Mkuu amesikiliza na kutolea maelekezo kero mbalimbali za wananchi ikiwemo migogoro ya ardhi, ndoa, huduma za kijamii na kuagiza viongozi wa serikali ngazi za wilaya kuzishughulikia kwa kuwa nyingi zilitakiwa kuishia huko.
Ametumia fursa hiyo, kusisitiza viongozi kusikiliza changamoto za watu na kuzitafutia majawabu.
Taarifa imesema ziara hiyo ya Kativu Mkuu wa CCM ni sehemu ya muendelezo wa utekelezaji wa maelekezo ya Halmashauri Kuu ya Taifa (NEC) ya kwa viongozi kuendelea kuwa karibu na wananchi, kuwasikiliza na kushughulikia changamoto zao.
Post a Comment