Featured

    Featured Posts

WAZIRI MKUU WA IRAQ: ZIARA YA ARUBAINI, IMEBEBA UJUMBE WA KUPINGA UHARIBIFU NA UFISADI

Adil Abdul-Mahdi aliyasema hayo Jumamosi kwa mnasaba wa marasimu ya Arubaini ya kuuawa shahidi Imam Hussein (as) ambapo sambamba na kulishukuru jeshi, idara za usalama, wizara za nchi hiyo na wanaowahudumia wafanyaziara kwa kujitolea kimatibabu na kwa chakula, amesisitiza kuwa uwepo wa mamilioni ya watu katika marasimu hayo, unaonyesha kuwa taifa la Iraq lipo huru na litaendelea kubakia hai.
Adil Abdul-Mahdi, Waziri Mkuu wa Iraq
Kadhalika Waziri Mkuu wa Iraq amebainisha kuwa nchi hiyo haiwezi kuhadaiwa na maadui. Ameendelea kubainisha kuwa, juhudi za wananchi katika kutoa huduma kwa wafanyaziara wa Arubaini ya Imam Hussein (as) zimeenda sambamba na juhudi na harakati endelevu za taifa na serikali kwa ajili ya kufanyika marekebisho na maendeleo,  ambalo ni jibu kwa matakwa halali ya taifa la Iraq, ya kupambana na ufisadi na kurejeshwa haki na fedha za taifa hilo. Adil Abdul-Mahdi amesema kuwa, ataendelea kushikamana na njia ya kukabiliana na nembo za ufisadi kwa kuwa ni lazima kuondolewe tofauti za kimatabaka kati ya wananchi na kuleta uadilifu wa kijamii. Jana tarehe 20 Swafar, 1441 Hijiria sawa na tarehe 19 Oktoba, ilisadifiana na Arubaini ya kuuawa shahidi katika jangwa la Karbala mjukuu wa Mtume (saw) yaani Imam Hussein (as) pamoja na wafuasi wasi wake wachache watiifu.
author

Author Name

Author Description!

Get Free Email Updates to your Inbox!

Post a Comment

www.CodeNirvana.in

Magazeti Ya Leo

Copyright © Magazeti ya Leo, Habari Leo Tanzania, Mwananchi, Michuzi, mwanaspoti, nipashe, Udaku | Designed By Code Nirvana