Bei ya korosho kwa mnada wa pili umeongezeka na kufikia 2717 kwa kilo moja ambapo mzigo wote uliopo tan 13,115 umeuzwa
Akitangaza Bei hiyo Meneja Mkuu wa TANECU Mohamed Mwinguku amesema kuwa korosho zilizopo kwenye maghala ya Chama Cha Ushirika Tandahimba na Newala (TANECU) zimenunuliwa zote
Amesema kuwa korosho kwa Wilaya ya Tandahimba imenunuliwa kwa sh 2717 kwa mnunuzi wa kwanza,wapili kanunua kwa sh 2697 na mnunuzi wa tatu amenunua kwa sh 2658
"Korosho iliyopo maghalani tayari tumeiuza yote kwa makampuni matatu Kati ya makampuni 37 yaliyojitokeza," amesema Mwanguku
Naye mkulima Hamis Hassan amesema pamoja na ongezeko Hilo malipo yafanyike kwa muda muafaka ili fedha zimfikie mkulima kwa wakati.
Katika mnada huo makampuni 37 na yalijitokeza,mnada mwingine wa tatu unatarajiwa kufanyika Wilaya ya Newala.
Meneja wa Chama Cha Ushirika Tandahimba na Newala (TANECU) Mohamed mwinguku akizungumza na w
Wadau wa zao la korosho wakifuatilia yaliyokuwa yakijiri ukumbini.
Post a Comment