Featured

    Featured Posts

KUWEKEWA VIKWAZO TAASISI ZA KIULINZI ZA IRANI

Taarifa iliyotolewa jana na Jeshi la Walinzi wa Mapinduzi ya Kiislamu imeeleza kuwa, vikwazo dhidi ya vikosi vya majeshi ya Iran na maafisa wa kijeshi wa nchi hii ambao siku zote wako  mstari wa mbele katika kudhamini usalama na kulifakharisha taifa hili mkabala na njama na mipango ya kishetani ya kambi ya maadui wa Mapinduzi ya Kiislamu ni ishara ya uhalali na mafanikio ya njia ya ufanisi, matumaini na fahari ya wananchi wa Iran na Umma mzima wa Kiislamu. Hatua hii katika upande mwingine imeivunja moyo na kuikatisha tamaa kambi ya adui hususan watawala wa White House. 
Makamanda wa Jeshi la IRGC

 
Tarehe 4 mwezi huu sambamba na maadhimisho ya Siku ya Taifa ya Kupambana na Ubeberu wa Kimataifa, ikulu ya Rais wa Marekani, White House, iliendeleza hatua zake za kukiuka sheria za kimataifa na za kihasama dhidi ya Iran na kuviwekea vikwazo vipya vikosi vya jeshi la ulinzi vya Jamhuri ya Kiislamu ya Iran. Vikwazo hivyo vimeongezwa katika faharasa ya vikwazo vya huko nyuma vya Marekani dhidi ya Iran. Vikosi vya ulinzi vya Iran vinavyolijumuisha Jeshi la Walinzi wa Mapinduzi ya Kiislamu (SEPAH) vina rekodi ya utendaji wa kujifakharisha wakati wa vita vya kujitetea kutakatifu na katika miaka yote ya baada ya vita vya kulazimishwa.  
Japokuwa moja ya malengo ya Marekani ya vikwazo hivyo ni kutaka kuficha kufeli mipango ya White House mbele ya irada na uwezo wa taifa la Iran, lakini hatupasi kupuuza nukta hii kwamba lengo kuu la Marekani la kuzilenga zaidi taasisi za kijeshi za Iran kwa silaha ya vikwazo ni kudhoofisha nafasi ya vikosi vya ulinzi vya Iran. Kwa mtazamo huo tunaweza kusema kuwa, vikwazo hivyo ni hatua yenye malengo matatu ya kistratejia.  
Lengo la kwanza ni kuidhirisha Iran kuwa tishio na hatari katika eneo la Mashariki ya Kati na katika uga wa kimataifa. Suala hilo lina umuhimu wa kistratejia katika kuendelezwa uingiliaji kati wa nchi za kibeberu katika masuala ya ndani ya nchi za eneo hilo na kuanzishwa miungano ya kijeshi ya Marekani. Hii ni katika hali ambayo masuala ya usalama ya eneo hilo yanapaswa kushughulikiwa na nchi za eneo husika. 
Lengo la pili ni kusababisha mgawanyiko na hitilafu kuhusiana na masuala ya kiusalama katika eneo la Mashariki ya Kati kupitia njia ya kuzifanya nchi za eneo zisishirikiane na Iran katika masuala ya ulinzi kwa kisingizio cha vikwazo. Hasa ikizingatiwa kuwa, Iran imewasilisha mpango wa pamoja kwa ajili ya kudhamini usalama katika eneo la Ghuba ya Uajemi. Akihutubia kikao cha Baraza Kuu la Umoja wa Mataifa huko New York, Rais Hassan Rouhani wa Jamhuri ya Kiislamu ya Iran aliwasilisha mpango wa amani ya kieneo chini ya anwani ya "Ubunifu wa Amani ya Hormuz" au "Muungano wa Matumaini." 
Lengo la tatu la vikwazo hivyo vya Marekani ni kukuza na kudhihirisha ukubwa wa vikwazo hivyo. Hata hivyo vikwazo hivyo havijawa na mafanikio kwa wale wanaoviweka.  
Meja Jenerali Mohammad Hossein Baqeri Mkuu wa Kamandi ya Majeshi yote ya Iran alisema hivi karibuni katika kikao cha makamanda na maafisa wa Jeshi la Walinzi wa Mapinduzi ya Kiislamu kwamba: Maadui wametambua kuwa vikosi vya ulinzi vya Iran viko tayari kukabiliana na maadui kwa azma na ushujaa na havitishwi wala kusita katika kutetea na kulinda malengo, ardhi na wananchi. 
Brigedia Jenerali Muhammad Baqeri, Mkuu wa Kamandi ya Majeshi yote ya Iran
 
Katika miaka 41 iliyopita Marekani imetumia njia nyingi kujaribu kuirejesha Iran katika kipindi cha kabla ya Mapinduzi ya Kiislamu na kuidhibiti tena nchi hii; hata hivyo imegonga mwamba katika njama yake hiyo. Vikwazo vya sasa vya Marekani pia vinakariri mahesabu yasiyo sahihi ya huko na mwisho wake ni kufeli na kugonga ukuta mkabala na Iran. 
author

Author Name

Author Description!

Get Free Email Updates to your Inbox!

Post a Comment

www.CodeNirvana.in

Magazeti Ya Leo

Copyright © Magazeti ya Leo, Habari Leo Tanzania, Mwananchi, Michuzi, mwanaspoti, nipashe, Udaku | Designed By Code Nirvana