Featured

    Featured Posts

WATU WATANO WAUAWA KWA MTETEMEKO WA ARDHI KASKAZINI MAGHARIBI MWA IRANI

Mtetemeko wa ardhi uliokuwa na ukubwa wa 5.9 kwa kipimo cha Rishta umetokea mapema leo Ijumaa katika wilaya ya Mianeh huko kaskazini magharibi mwa Iran na kuua watu wasiopungua 5.
Mkuu wa Shirika la Huduma za Haraka za Matibabu katika Mkoa wa Azerbaijan Mashariki, Farzad Rahman amesema kuwa, watu wengine 20 wamejeruhiwa katika mtetemeko huo wa ardhi.
Mtetemeko huo uliokuwa na 5.9 kwa kipimo cha Rishta umeathiri zaidi kijiji cha Varnakesh eneo la Tark ambako watu 5 wameuawa na nyumba 30 zimeharibiwa. Mtetemeko huo wa ardhi umetokea umbali wa kilomita 10 chini ya ardhi na kufuatiwa na mitetemeko mingine 60 hafifu.  Watu milioni 20 wa maeneo ya kaskazini magharibi mwa Iran na nchi jirani ya Uturuki wamehisi mtetemeko huo. 
Kikosi cha kujitolea cha Basij na Jeshi la Walinzi wa Mapinduzi ya Kiislamu (IRGC) kimetumwa katika eneo hilo kwa ajili ya kusaidia juhudi za uokoaji. 
Juhudi za uokoaji zinaendelea
Rais Hassan Rouhani wa Iran amemtaka gavana wa mkoa wa Azarbaijan Mashariki na maafisa wa serikali mkoani huko kutumia nyenzo zote kwa ajili ya kuwaidia watu waliopatwa na maafa hayo. Vilevile amemtuma Waziri wa Viwanda, Madini na Biashara, Reza Rahmani katika neo hilo kwenda kusimamia zoezi la uokoaji na misaada ya dharura kwa watu waliopatwa na maafa. 
author

Author Name

Author Description!

Get Free Email Updates to your Inbox!

Post a Comment

www.CodeNirvana.in

Magazeti Ya Leo

Copyright © Magazeti ya Leo, Habari Leo Tanzania, Mwananchi, Michuzi, mwanaspoti, nipashe, Udaku | Designed By Code Nirvana