Featured

    Featured Posts

CCM YAANZA MCHAKATO WA KUANDIKA MWELEKEO WA SERA ZAKE 2020/2030 NA UUNDAJI WA ILANI YA UCHAGUZI 2020, YATOA NAFASI KWA WADAU KUCHANGIA MAONI

NA BASHIR NKOROMO, DAR ES SALAAM
Chama Cha Mapinduzi (CCM) kimeanza mchakato wa kuandika Mwelekeo wa Sera zake kwa mwaka 2020 hadi 2030 na uundaji wa Ilani ya Uchaguzi kwa Mwaka 2020 hadi 2025, huku kikitoa nafasi kwa wadau kuchangia maoni yao kwa ajili hiyo.

Taarifa iliyotolewa na Katibu wa Halmashauri Kuu ya Taifa (NEC) ya CCM, Idara ya Itikadi na Uenezi Humphrey Polepole, imesema tayari CCM imeshaanza mchakato huo kupitia Kamati ya Uandishi wa Mwelekeo wa Sera na Ilani ya CCM ambayo ipo chini ya Mwenyekiti wake, Makamu wa Mwenyekiti wa CCM Tanzania Bara Phillip Mangula na kwamba   Kamati hiyo inaomba maoni ya wadau yawe yameifikia Kamati kabla ya Tarehe 25 Januari 2020.

 "Kama ilivyo desturi ya Chama Cha Mapinduzi (CCM) katika michakato yake yote ya uaandaji nyaraka muhimu za Chama ikiwamo mwelekeo wa Sera na Ilani ya Uchaguzi msingi mkuu huwa ni ushiriki na ushirikishaji wa umma wa Watanzania na wanachama wa CCM kote nchini. Msingi huu wa kushirikisha umma unatokana na asili ya Chama ya Chama Cha Mapinduzi ambayo ni vitu viwili, kutenda haki na kuheshimu watu", amesema Polepole katika taarifa hiyo.

Amesema CCM inawakaribisha mtu mmoja mmoja au vikundi vya watu na taasisi mbalimbali ikiwemo Vyama vya Wafanyakazi, Wawakilishi wa vyama vya Wakulima, Vyama vya siasa vyenye usajili wa kudumu, Vyama vya Waalimu, Wachimbaji wadogo wadogo wa madini, wafanyabiashara wa madini, wawakilishi na vyama vya wakulima.

Wengine ni wavuvi na wafugaji, jumuia za machinga na wasafirishaji wadogo wadogo kama bodaboda na bajaji, Jumuia za Wanawake, Watu wenye ulemavu, Vijana, Wazee, Watoto, Asasi zisizokuwa za Kiserikali, Wasomi, Wanafunzi wa Vyuo na Vyuo Vikuu, Wadau na wana Tasnia ya Sanaa, Burudani na Michezo, wasafirishaji wa mizigo na abiria, wenye viwanda, wadau wa sekta ya utalii na vyama vya ushirika kwa maeneo yao.

Polepole amesema, kwa upande wadau ambao ni wanachama wa Chama Cha Mapinduzi, Kamati za Siasa za Mikoa na Wilaya ziweke utaratibu wa kukusanya maoni na kuwasilisha Makao Makuu kama ambavyo imekwisha kuelekezwa.

Polepole amesema Maoni yanaweza kuwasilishwa kwa Katibu Mkuu wa CCM, Makao Makuu ya CCM, S.L.P 50, Dodoma, Ofisi Ndogo ya Makao Makuu ya CCM, S.L.P 9151, Dar es Salaam, Afisi Kuu ya CCM, Kisiwandui, Zanzibar au kwa baruapepe: katibumkuu@ccm.or.tz na 
pia yanaweza kuwasilishwa kwa Polepole mwenyewe ambaye ni Katibu wa Kamati ya Wataalam kwa kupitia baruapepe: hpolepole@hpolepole.com

Polepole amemaliza taarifa hiyo kwa kusema, "uongozi wa Chama Cha Mapinduzi (CCM) chini ya Mwenyekiti wake, Rais Dk. John Magufuli,  unapenda kuwatakia wana CCM na Watanzania wote Heri ya Mwaka Mpya, Mwaka 2020 ukawe wenye Baraka, Amani, umoja, neema, mafanikio na kuinuliwa kwa mtu mmoja mmoja na Taifa la Tanzania, sote tukafanye kazi kwa bidii na huu ukiwa ni msingi wa kulinda utu na uhuru wa Taifa letu".
author

Author Name

Author Description!

Get Free Email Updates to your Inbox!

Post a Comment

www.CodeNirvana.in

Magazeti Ya Leo

Copyright © Magazeti ya Leo, Habari Leo Tanzania, Mwananchi, Michuzi, mwanaspoti, nipashe, Udaku | Designed By Code Nirvana