Jeshi la Polisi wilayani Handeni mkoani Tanga, limemkamata Mwenyekiti wa Chama cha Wananchi CUF, Profesa Ibrahimu Lipumba, kwa madai ya kufanya ziara bila kuwa na kibali.
Profesa Lipumba amekamatwa leo Jumapili Januari 26, 2020 Kijiji cha Segera wilayani Handeni na kupelekwa kituo kikuu cha polisi wilayani humo kilichopo mjini Handeni.
Mkurugenzi wa Usalama wa CUF, Masoud Mhina amesema mwenyekiti huyo amekamatwa wakati akijiandaa kufungua tawi la chama hicho Kijiji cha Segera.
Amesema ameshangazwa na kitendo hicho cha polisi kumkamata Profesa Lipumba wakati tayari chama kilishawasilisha jeshi la polisi taarifa ya ziara hiyo.
Taarifa zaidi zitafuata, juhudi za kumtafuta RPC Tanga zinaendelea.
Post a Comment