Featured

    Featured Posts

ASKARI POLISI AKATWA SEHEMU ZA SIRI NA MKEWE

   Mwanamke mmoja aliyefahamika kwa jina la Flora Adam (23) anashikiliwa na Jeshi la Polisi Mkoa wa Shinyanga , kwa tuhuma za kumkata mume wake sehemu zake za siri kisa wivu wa kimapenzi.

Mwanaume huyo aliyenusurika kifo amefahamika kwa jina la  Kazimir (28) ambaye ni Askari polisi.


Kamanda wa Polisi mkoani humo Deborah Magiligimba, amesema kuwa tukio hilo lilitokea Disemba 28, 2019, majira ya saa 6:00 usiku, wakati wakiwa wamelala ambapo ghafla mwanamke huyo alinyanyuka kitandani na kumkata mume wake na kitu chenye ncha kali sehemu zake za siri.

Baada ya tukio hilo Askari huyo, alikimbizwa katika Hospitali ya rufaa ya Serikali ya Mkoa wa Shinyanga, ambako alilazwa kwa siku mbili na badaye aliruhusiwa.
author

Author Name

Author Description!

Get Free Email Updates to your Inbox!

Post a Comment

www.CodeNirvana.in

Magazeti Ya Leo

Copyright © Magazeti ya Leo, Habari Leo Tanzania, Mwananchi, Michuzi, mwanaspoti, nipashe, Udaku | Designed By Code Nirvana