Featured

    Featured Posts

HALI YA SHEIKH ZAKZAKY KUZIDI KUWA MBAYA CHINI YA MASHINIKIZO SERIKALI YA NIGERIA

Ofisi ya Sheikh Zakzaky imetangaza katika ukurasa wake wa Twitter kwamba: taarifa ilizopokea kutoka kwa watu waliomtembelea Kiongozi huyo wa Harakati ya Kiislamu ya Nigeria zinaonyesha kuwa hali ya kiafya ya Sheikh Zakzaky imezidi kuwa mbaya. Hii ni katika hali ambayo wakuu wa jela wanaendelea kuwazuia madaktari ya kumuona kiongozi huyo wa kidini. 
Sheikh Ibrahim Zakzaky na mkewe walitiwa mbaroni Disemba 13 mwaka 2015 katika Husseiniya ya mji wa Zaria nchini Nigeria. Ni zaidi ya miaka minne sasa imepita tangu Sheikh Zakzaky na mkewe walipokamatwa na wanajeshi wa Nigeria na hadi hivi sasa wanaendelea kushikiliwa jela; huku wanajeshi wa nchi hiyo wakiendeleza mashinikizo dhidi ya Waislamu wa nchi hiyo. Hata hivyo licha ya mashinikizo yote hayo, Waislamu wa Nigeria katika miezi ya karibuni wamefanya maandamano mara kadhaa katika miji mbalimbali ya nchi hiyo wakitaka kuachiwa huru Sheikh Zakzaky. Pamoja na hayo lakini serikali ya Nigeria si tu haisikilizi matakwa ya haki ya wananchi hao, bali askari usalama wa nchi hiyo nao wamekuwa wakikandamiza kikatili maandamano hayo ya Waislamu.   
Sheikh Ibrahim Zakzaky picha ya kulia baada ya kujeruhiwa mwaka 2015 na wanajeshi wa Nigeria katika mji wa Zaria 
Kiujumla hali ya Sheikh Ibrahim Zakzaky inazidi kuwa mbaya siku baada ya siku ambapo kabla ya ripoti hii, Ofisi ya Harakati ya Kiislamu ya Nigeria ilitahadharisha kuhusu hali ya kimwili na kuzidi kuugua mwanazuoni huyo. Hata kama Sheikh Zakzaky mwezi Agosti mwaka jana alisafirishwa kwenda India kwa ajili ya matibabu kutokana na mashinikizo ya Waislamu wa nchi hiyo, lakini kutoandaliwa mazingira ya kupatiwa matibabu na kushindwa India kutoa ushirikiano katika uwanja huo kulimlazimisha Sheikh Zakzaky arejee Nigeria; na tangu wakati huo hadi sasa mwanazuoni huyo anashikiliwa na wanajeshi wa nchi hiyo. 
Ukweli wa mambo ni kuwa kwa kumshikilia korokoroni Sheikh Zakzaky; serikali ya Nigeria inajaribu kuiweka chini ya mashinikizo Harakati ya Kiislamu ya nchi hiyo na kuwatenga mbali na uga  wa kisaisa Waislamu wa nchi hiyo. Waislamu hao katika miaka kadhaa ya karibuni wamekuwa na nafasi kuu kwenye masuala ya kisiasa na kijamii nchini Nigeria chini ya uungaji mkono wa Sheikh Ibrahim Zakzaky; suala ambalo lilihesbiwa kama tishio kuu kwa serikali ya Nigeria na wiatifaki wake ambao wamekuwa wakifanya kila linalowezekana kuwa na ushawishi nchini humo na barani Afrika kiujumla. Viongozi wa Nigeria hasa baadhi ya viongozi wa ngazi ya juu wa kijeshi wa nchi hiyo wamethirika pakubwa na siasa na matakwa ya utawala wa Kizayuni na Saudi Arabia kwa sababu mbalimbali kama kuhongwa fedha na kusaidiwa kisiasa na tawala hizo; na ndio maana wanachukua hatua dhidi ya Waislamu wa NIgeria katika kalibu ya siasa hizo. 
Sheikh Ibrahim Zakzaky na mkewe walipokuwa India 
Masoud Shajare Mkuu wa Kituo cha Kiislamu cha Haki za Binadamu cha mjini London anasema kuhusiana na suala hilo kwamba: Serikali ya Nigeria inafanya juhudi kwa kutumia kila mbinu kumuuwa Sheikh Zakzaky na kuiangamiza harakati yake ili kuandaa mazingira ya kurejesha nguvu ya ubepari wa Magharibi barani Afrika.  
Kwa kuzingatia hali mbaya ya kimwili ya Sheikh Zakzaky; kuendelea kushikiliwa kwake kunaweza kuwa na athari mbaya kama kumsababishia kifo. Hii ni katika hali ambayo viongozi wa Nigeria si tu wanakaidi kuachiwa huru Sheikh Zakzaky bali wanataka kuendesha kesi dhidi yake na kumzushia tuhuma mpya mwanachuo huyo. 
Kama alivyosema Aisha Dikko Mwanasheria Mkuu wa Kaduna kwamba hatima ya Sheikh Zakzak ipo mikononi mwa mahakama na si kwa serikali ya jimbo. 
Ofisi ya Sheikh Zakzaky kwa upande wake imetangaza kwamba: Hapana shaka kuwa mdhalimu wana malengo ya hatari nyuma ya pazia na lengo lao ni kumdhuru Sheikh huyo mgonjwa. Ni dhahir shahir kuwa viongozi wa Nigeria wamekusudia kutumia mahakama kutekeleza lengo lao kuu yaani kumhukumu kunyongwa  Sheikh Zakzaky.  
Aisha Dikko, Mwanasheria Mkuu wa Kaduna 
Wakati huo huo Waislamu wa Nigeria wamesisitiza kulindwa malengo ya Kiislamu na kusema kuwa kumshikilia Sheikh Zakzaky katika mazingira kama hayo si kitendo cha uadilifu na ni katika njama iza kumdhoofisha kimwili kiongozi huyo. Waislamu hao aidha wametahadharisha kuhusu taathira za maamuzi kama hayo ya viongozi wa Nigeria. Ofisi ya Sheikh Zakzaky imeandika katika ukurasa wake wa Twitter kwamba: Taathira za hatua hizo kubwa zisizo za kiadilifu zinaweza kuwa hatari sana, zisizotabirika na zisizoweza kufidiwa ndani na nje ya Nigeria.
author

Author Name

Author Description!

Get Free Email Updates to your Inbox!

Post a Comment

www.CodeNirvana.in

Magazeti Ya Leo

Copyright © Magazeti ya Leo, Habari Leo Tanzania, Mwananchi, Michuzi, mwanaspoti, nipashe, Udaku | Designed By Code Nirvana