Mwenyekiti wa Baraza la Utendaji la Harakati ya Hizbullah ya Lebanon amesisitiza kuhusu kuondoka wanajeshi wa Marekani katika eneo la Asia Magharibi kama jibu la kweli la mauaji ya kigaidi ya mashahidi Haj Qassem Soleimani na Abu Mahdi al Muhandis.
Kwa mujibu wa taarifa, Sayyid Safiuddin ameyasema hayo katika hafla iliyofanyika katika eneo la Deir Qanun Al Nahr kusini mwa Lebanon na kuongeza kuwa: "Baada ya kuuawa shahidi viongozi na makamanda wetu, hatukuwa na shaka hata kidogo kuwa Israel imeshindwa na itashindwa."
Aidha amesisitiza kuwa, leo hakuna shaka kuwa viongozi wa muqawama watakamilisha mkondo huu na Marekani itaondoka katika eneo.
Safiuddin ameendelea kusema kuwa, siku, wiki na miezi ijayo Marekani itapata pigo kubwa na hali ya Marekani haitakuwa kama ilivyokuwa huko nyuma.
Baada ya jinai ya Marekani ya kuwaua kigaidi Luteni Jenerali Qassem Soleimani, Kamanda wa Kikosi cha Quds cha Jeshi la Walinzi wa Mapinduzi ya Kiislamu na Abu Mahdi al Muhandis, Naibu Kamanda wa Al Hashd al Shaabi na wanamapambano wanane waliokuwa wameandamana nao, kuondoka askari wa kigaidi wa Marekani katika eneo ni takwa muhimu zaidi la makundi ya muqawama.
Post a Comment