Mwakilishi wa Ofisi ya Kisiasa ya Harakati ya Jihadul Islami ya Palestina amesema kuwa maamuzi yasiyo sahihi ya Rais Donald Trump wa Marekani kuhusu mpango wa "Muamala wa Karne" hayana thamani yoyote. Amesema kuwa mpango huo hautakwamisha mapambano ya wananchi wa Palestina.
Sheikh Nafidh Azzam amesisitiza kuwa "Mpango wa Muamala wa Karne" hautatekelezwa na kuongeza kuwa ni njozi kudhani kwamba, hatima ya Quds itakwua mikononi mwa kundi lisilo la Waislamu.
Mpango wa kishetani uliobuniwa na Marekani na Wazayuni wa Israel uliopewa jina la Muamala wa Karne unatazamiwa kuzinduliwa katika kikao cha Jumenne ijayo Januari 28 kati ya Rais Donald Trump wa Marekani na Benjamin Netanyahu Waziri Mkuu wa utawala wa Kizayuni. Kwa mujibu wa mpango huo, Quds Tukufu itakabidhiwa kwa utawala wa Kizayuni, wakimbizi wa Kipalestina hawatakuwa tena na haki ya kurejea katika ardhi za mababu zao na Palestina itamiliki tu aradhi zilizosalia huko katika Ukingo wa Magharibi mwa Mto Jordan na Ukanda wa Ghaza.
Rais Donald Trump Disemba Sita mwaka 2017 aliutangaza mji wa Quds unaokaliwa kwa mabavu kuwa mji mkuu wa utawala bandia wa Israel katika fremu ya mpango wa Muamala wa Karne na akatangaza uamuzi wake wa kuuhamisha ubalozi wa Marekani kutoka Tel Aviv hadi Quds. Serikali ya Marekani Mei 14 mwaka juzi ilitekeleza uamuzi huo. Itakumbukwa kuwa mji wa Quds unakaliwa kwa mabavu na utawala wa Kizayuni tangu mwaka 1967.
Post a Comment