Featured

    Featured Posts

KOCHA YANGA APEWA ONYO, WATANO WAFUNGIWA MECHI TATU



Kocha wa Yanga Luc Eymael amepewa onyo Kali kwa matamshi aliyoyatoa kuhusu ubaguzi wa rangi katika mchezo dhidi ya Azam FC uliopigwa Januari 18, 2020 na kushuhudia mchezo huyo ukimalizika kwa Yanga kufungwa goli 1-0.

Maamuzi hayo yametolewa na kamati ya Uendeshaji wa Ligi (Kamati ya Saa 72) leo katika ofisi za TFF Jijini Dar es Salaam.

Kamati ya Uendeshaji na Usimamizi wa Ligi ya Bodi ya Ligi Kuu Tanzania (TPLB) imempa onyo Kocha wa Klabu ya Yanga, Luc Eymael kwa kufanya vitendo na kutoa matamshi yasiyofaa.

Aidha kamati hiyo imeitaka klabu ya Yanga kutoa tamko juu ya kauli hizo pamoja na vitendo vingine alivyoeleza kuwa siyo vya kiungwana.

Katika adhabu nyingine, Klabu ya Tanzania Prisons na Yanga zimepigwa faini ya Tsh. 500,000 kila mmoja kwa kutokuwakilisha Vikosi vya Timu kwenye kikao cha maandalizi katika mchezo wao wa Desemba 29, 2019

Klabu ya Yanga imetozwa faini ya Tsh. 500,000 kutokana na Washabiki wake kurusha chupa za maji kuelekea uwanjani na wakati wa mapumziko waliwarushia chupa za maji Waamuzi

Vile vile katika mchezo huo Klabu ya Yanga imepigwa faini ya Tsh. 200,000 kwa kutokutumia Chumba Rasmi kilichoandaliwa kwa kubadilishia nguo

Aidha, Wachezaji wa Mbeya City (Kelvin John na Majaliwa Shaban) na Yanga (Mrisho Ngasa, Ramadhani Kabwili na Cleafas Sospeter) kila mmoja amefungiwa michezo mitatu na kupigwa faini ya Tsh. 500,000 kila mmoja kwa kugoma kuingia vyumbani

Kamati imeeleza kuwa katika adhabu za wachezaji waliofungiwa hususani wa Yanga watatumika katika mchezo wa leo mpaka pale Klabu zao watapopata barua kutoka Bodi ya Lig
author

Author Name

Author Description!

Get Free Email Updates to your Inbox!

Post a Comment

www.CodeNirvana.in

Magazeti Ya Leo

Copyright © Magazeti ya Leo, Habari Leo Tanzania, Mwananchi, Michuzi, mwanaspoti, nipashe, Udaku | Designed By Code Nirvana