Featured

    Featured Posts

MAAMBUKIZI YA UKOMA YAPUNGUA KUTOKA WATU 43 HADI 26

  Na.Faustine Gimu Galafoni,Dodoma
Katika kuelekea Maadhimisho ya siku ya Ukoma Duniani leo,Waziri wa Afya Maendeleo ya Jamii,Jinsia Wazee na Watoto ,Mhe.Ummy Mwalimu amesema kiwango cha maambukizi mapya ya ugonjwa wa ukoma umepungua kutoka watu 43 kati ya watu milioni  Moja  2014 hadi watu kufikia wagonjwa 26 kati ya watu milioni Moja mwaka 2019.


Amezungumza hayo jana jijini Dodoma alipokuwa akizungumza na wazee ambao ni waathirika wa ugonjwa wa ukoma katika kijiji cha Samaria Kata ya Hombolo bwawani.

Amesema kupungua kwa maambukizi hayo ni kutokana  na juhudi zaa serikali za kuhakikisha  wanapima na kutoa matibabu bure kwa aathirika wa ugonjwa wa huo.

Pia Waziri Ummy amesema maambukizi mapya Ukoma kwa watoto takriban asilimia 41 % ambapo mwaka 2014 kulikuwa na watoto 90  na wamepungua hadi watoto  53 mwaka 2019.

Kwa upande wake mkurugenzi wa progamu  wa elimu vijini (CHEP) Ruteni Kanal  Msaafu Daudi Tandila  amesema  Kulingana na Takwimu hizo,na msimamo wa shirika la afya Duniani (WHO) yakuwa Kati ya wagonjwa elfu kumi akipatikana Mgonjwa Mmoja,italeta ripoti ya kuwa hakuna ugonjwa wa ukoma.

Hivyo Wizara ya afya ikusanye taarifa upya kupata Takwimu zinazotolewa na WHO za udhibitisho wa Kutokuwepo kwa ugonjwa huo.

Sambamba na hayo Waziri Ummy amekabidhi sukari kilo 50,Mchele kilo 100,maharage kilo 50,unga kilo 50 na viatu pea 48 kwa waathirika wa Ukoma  kama ishara ya kuwathamini huku  akishikana mikono nao  katika kupinga dhana potofu  ya kwamba ugonjwa huo unaambukiza   kwa njia ya kushikana.

Kuhusu changamoto ya miundombinu ya barabara iliyopo katika eneo hilo Waziri Ummy amemwagiza mkuu wa wilaya alifanyie kazi kwani imekuwa kero na changamoto kubwa ambapo ilisababisha msafara wake kukwama mara kwa mara hali iliyomsababisha kutembea kwa miguu.
author

Author Name

Author Description!

Get Free Email Updates to your Inbox!

Post a Comment

www.CodeNirvana.in

Magazeti Ya Leo

Copyright © Magazeti ya Leo, Habari Leo Tanzania, Mwananchi, Michuzi, mwanaspoti, nipashe, Udaku | Designed By Code Nirvana