Wakati huo huo, mataifa kote duniani yanapanga kuwaondoa wafanyakazi wao wa kibalozi pamoja na raia kutoka maeneo ya China yaliokumbwa na virusi vya Corona vinavyosambaa kwa haraka.
Mji wa Wuhan ulio na takriban watu milioni 11 katika mkoa wa Hubei na kitovu cha mripuko huo, umewekwa chini ya masharti magumu ya raia wake kutosafiri.
Waziri wa mambo ya nje wa Japan Toshimitsu Motegi amesema taifa hilo litatuma ndege mjini Wuhan siku ya Jumanne yenye uwezo wa kubeba abiria 200 na kuongeza kuwa takriban watu 650 wanatarajia kurejea Japan.
Ujerumani itawaondoa raia wake 90 wanaoishi katika eneo la Wuhan na Kazakhstan nayo imeiambia China kuwaruhusu wanafunzi wake 98 kuondoka mjini Wuhan.
Post a Comment