Wizara ya Maji ya Misri imetangaza kuwa, mazungumzo yaliyokuwa yakiendelea huko Addis Ababa kati ya nchi hiyo, Ethiopia na Sudan kuhusiana na bwawa na al-Nahdha yamevunjika baada ya pande husika kushindwa kufikia makubaliano.
Taarifa ya Wiizara ya Maji ya Misri imeeleza kuwa, Ethiopia haijaeleza hatua za kueleweka kwa ajili ya kulinda uwezo wa bwawa la al-Nahdha mkabala na matukio tarajiwa ya kujazwa maji katika bwawa hilo.
Wawakilishi wa Misri, Sudan na Ethiopia walikutana kwa siku mbili huko Addis Abab kwa ajili ya kujadiliana kuhusiana na masuala mbalimbali ambapo licha ya matumaini makubwa iliyokuwa Cairo ya kuwa na matunda kikao hicho, lakini pande husika zimeshindwa kufikia makubaliano kuhusiana na masuala zinayotofautiana.
Serikali ya Misri ilikuwa imetangaza kabla ya kikao hicho kwamba, kuna matumaini wa kufikiwa makubaliano baina ya pande husika kabla ya tarehe 15 mwezi huu wa Januari.
Bwawa la An-Nahdha linaendelea kujengwa juu ya Mto wa Blue Nile na katika eneo lenye urefu wa kilomita 40 katika mpaka wa pamoja wa Ethiopia na Sudan.
Serikali ya Misri inaamini kuwa asilimia 90 ya mahitaji ya maji ya nchi hiyo inadhaminiwa na maji matamu ya Mto Nile na kwamba baada ya bwawa la al-Nahdha kujazwa maji kikamilifu nchi hiyo itakabiliwa na matatizo makubwa ya uhaba wa maji.
Post a Comment