Featured

    Featured Posts

MKOA WA KAGERA WAJIPANGA KUONDOKANA NA UDUMAVU

 Kaimu Mkurugenzi wa Halmashauri ya wilaya ya Bukoba mkoani Babylus Mashauri akifungua kikao cha Elimu juu ya matumizi ya vyakula ili kuondokana na tatizo la udumavu kwa watoto.
Afisa lishe Halmashauri ya wilaya ya Bukoba mkoani Kagera Desdery Karugaba akizunguza na wadau wakati alipokuwa katika kikao cha Elimu juu ya matumizi ya vyakula ili kuondokana na tatizo la udumavu kwa watoto.

Na Lydia Lugakila Kagera:-
Halmashauri ya wilaya ya Bukoba mkoani yajipanga kutoa Elimu juu ya matumizi ya vyakula ili kuondokana na tatizo la udumavu kwa watoto.

Kauli hiyo imetolewa na wadau wa kikao lishe kilichofanyika katika ukumbi wa mikutano wa Halmashauri ya wilaya ya Bukoba mkoani Kagera.

Akifungua katika kikao hicho kaimu mkurugenzi wa Halmashauri ya Bukoba mkoani Kagera Babylus Mashauri ametaka kujua ni kwa nini mkoa huo wenye upatikanaji  wa vyakula vingi mboga mboga za kutosha unakabiliwa na tatizo la Udumavu.

Wadau hao kwa pamoja wakabaini kuwa bado kuna changamoto kubwa ya baadhi ya kaya kutokuwa na Elimu juu ya matumizi ya vyakula walivyonavyo jambo linalosabisha kuwepo kwa tatizo la udumavu.

Mashauri amesema mikakati ya kuhakikisha udumavu unafutika inatakiwa kupitia utoaji elimu kwa kila kaya na kudai kuwa haiwezekani  kuona mkoa wa Kagera wenye vyenye tiba ya udumavu unakumbwa na janga hilo.

Anord Mutafungwa ni Afisa wa ufuatiliaji wa Tathimini Mkoani Kagera amekiri kuwa elimu ndogo ni changamoto kwa baadhi ya  kaya kwani katika msimu wa kuvuna mazao kaya hizo uuza chakula chote na kubaki na akiba kidogo huku watoto wakikosa Milo mitatu hivyo akakubaliana na wadau kutolewa kwa elimu ya matumizi ya vyakula.

Kwa upande wake afisa lishe wa Halmashauri ya wilaya ya Bukoba Mkoani Kagera Desdery Karugaba amesema mikakati ya pamoja inahitajika ili kuiongezea uwezo jamii ili kuondokana na tatizo hilo.

Karugaba amesema suala la Mtoto kudumaa linahusisha vitu vingi sana ikiwa ni ukosefu wa vyakula hitajika.

Hata hivyo afisa lishe amewahimiza akina mama kuwa katibu na watoto wao hasa katika suala la ulishaji wa chakula ambao ni shirikishi kuliko.

Hata hivyo ametoa wito kwa jamii kuzingatia usafi wa mazingira ili kuepukana na magonjwa ya mlipuko.
author

Author Name

Author Description!

Get Free Email Updates to your Inbox!

Post a Comment

www.CodeNirvana.in

Magazeti Ya Leo

Copyright © Magazeti ya Leo, Habari Leo Tanzania, Mwananchi, Michuzi, mwanaspoti, nipashe, Udaku | Designed By Code Nirvana