Mtunukiwa wa Tuzo ya Heshima ya Udaktari (PhD) Mkurugenzi Mtendaji wa Tanzania Horticultural Association (TAHA), Dkt. Jaquelin Mkindi, akiwa katika mahafali ya 39 ya Chuo cha Africa Graduate University yaliyofanyika jijini Arusha hivi karibuni.Mtunukiwa wa Tuzo ya Heshima ya Udaktari (PhD) Mkurugenzi Mtendaji wa Tanzania Horticultural Association (TAHA), Dkt. Jaquelin Mkindi, akihutubia baada ya kutunukiwa tuzo hiyo. Mtunukiwa wa Tuzo ya Heshima ya Udaktari (PhD) Mkurugenzi Mtendaji wa Tanzania Horticultural Association (TAHA), Dkt. Jaquelin Mkindi, akiingia ukumbini.
Mtunukiwa wa Tuzo ya Heshima ya Udaktari (PhD) Mkurugenzi Mtendaji wa Tanzania Horticultural Association (TAHA), Dkt. Jaquelin Mkindi (wa tatu kulia waliokaa) akiwa katika picha ya pamoja na mgeni rasmi na waalikwa wengine baada ya kutunukiwa tuzo hiyo.
………………………………………….
Na Dotto Mwaibale
CHUO cha Africa Graduate University Kampasi ya Uingereza kimemtunuku Tuzo ya Heshima ya Udaktari (PhD) Mkurugenzi Mtendaji wa Tanzania Horticultural Association (TAHA), Dkt. Jaquelin Mkindi.
Waliotunukiwa tuzo hizo za heshima ni wale waliotoa mchango mkubwa kwa kufanya shughuli mbalimbali za kujitolea za kijamii na zikaleta manufaa kwa mtu mmoja mmoja na taifa kwa ujumla.
Akizungumza wakati wa mahafali ya 39 ya chuo hicho, Makamu Mkuu wa Chuo hicho chenye makao makuu yake nchini Sierra Leone, Profesa Timothy Kazembe, alisema kila mwaka kimekuwa kikitoa Tuzo za heshima na Shahada za Uzamili kwa watanzania waliotoa mchango wa kusaidia jamii katika shughuli mbalimbali.
“Tunao watunuku tuzo hizi tuzo za heshima ni watu waliokuwa na umri wa miaka 60 ambao wanafanya kazi za kijamii katika nyumba za ibada kwa zaidi ya miaka 15 na kuendelea na wale ambao umri wao ni miaka 40 hadi zaidi na wenye shahada” alisema Profesa Kazembe.
Mkindi ametunukiwa Tuzo hiyo kutokana na mchango wake mkubwa katika jamii kwani ndiye mwanzilishi wa Taasisi isiyo ya kiserikali ambayo inafanya vizuri katika masuala ya kilimo hapa nchini.
Katika mahafali hayo yaliyofanyika Hoteli ya Gran Melia jijini Arusha na kupambwa na Bendi ya Jeshi la Polisi kutoka Chuo cha Polisi (CCP) yalihudhuriwa na watu maarufu na mgeni rasmi alikuwa ni Makamu Mkuu wa Chuo cha Nelson Mandela African Institute of Science and Technology, Profesa Emmanuel Luoga
Post a Comment