Akizungumza na waandishi wa habari jijini Dodoma Mwenyekiti wa timu hiyo Mhe.Rashid Shangazi amesema kuwa uzinduzi huo utaambatana na uzinduzi wa kadi za mashabiki, wapenzi pamoja na wanachama maeneo ya Equity Bank tawi la Dodoma lililopo Uhindini. Kulia ni Mhamasishaji wa klabu hiyo Mbunge wa Sengerema Mhe.William Ngeleja
Aidha Mhe.Shangazi amesema kuwa katika tukio kubwa na la kihistoria kwa wabunge kuwa na Tawi amewaomba watani zao Yanga kujumuika nao ili nao waweze kujifunza hata kuiga mambo yaliyo mazuri.
”Tumewaalika mashabiki wote wa Yanga akiwemo Waziri Mhe.George Mkuchika ambaye ni Mdhamini wa Yanga,Mbunge wa Dodoma Mhe.Anthony Mavunde,Freeman Mbowe pamoja na Kamanda wa Polisi Mkoa wa Dodoma Muroto”amesema Shangazi.
Naye Mhamasishaji wa klabu hiyo Mbunge wa Sengerema Mhe.William Ngeleja,amewaomba mashabiki na wapenzi pamoja na wanachama wote kanda ya Dodoma kujitokeza kwa wingi kwenye tukio hili muhimu kwa faida ya timu. Kulia ni Mbunge wa Viti Maalum mkoa wa Shinyanga Mhe. Salome Makamba
”Dunia kitu kinachopendwa zaidi ni mpira wa mguu na sisi kama mashabiki wa Simba tumekuwa wabunge wa kwanza nchini pamoja na Duniani kuwa na Tawi jipya na la Kisasa”
Mbunge wa Viti Maalum mkoa wa Shinyanga Mhe.Salome Makamba,amesema kuwa Simba ni klabu kubwa na yenye mafanikio hapa nchini hivyo wameamua kuiunga mkono katika uzinduzi huu wa tawi pamoja na ugawaji wa Kadi kwa Mashabiki. kushoto ni Mhamasishaji wa klabu hiyo Mbunge wa Sengerema Mhe.William Ngeleja
Kwa upande wa klabu ya Simba wataongozwa na Mtendaji Mkuu Senzo Mbatha pamoja na Msemaji wa klabu hiyo kipenzi cha wanasimba Haji Manara atakuwepo kwa ajili ya kuhamasisha zoezi hilo la kihistoria
Post a Comment