Magazeti ya Leo, Habari Leo Tanzania, Mwananchi, Michuzi, mwanaspoti, nipashe, Udaku

Magazeti ya leo, gazeti la mwananchi, global publisher, habari leo, habari mpya, ippmedia,magazeti ya leo tanzania, magazeti ya udaku, michuzi, michuzi blog, mpekuzi huru, mwananchi, mwanaspoti,nipashe, sekretarieti ya ajira

MENU
  • HOME
  • Drop Down 1
    • Element 1
    • Element 2
    • Element 3
  • Option 1
  • Option 2
  • Drop Down 2
    • Element 1
    • Element 2
    • Element 3
    • Element 4
  • Contact Us
Featured

    Featured Posts

PROF. MUHONGO AZINDUA SHULE BINAFSI YA AGAPE YA MZAWA WA KIJIJI CHA BUKIMA, KAYOLE MUSOMA VIJIJINI

on 08/01/2020 Brown Alex
Wanafunzi, Walimu, Wazazi, Viongozi wa Serikali na Chama (CCM) wamehudhuria SHEREHE za UZINDUZI wa AGAPE Primary School zilizofanyila Jumanne, 7.1.2020 Kijijini Bukima.
KIONGOZI na MMLIKI wa Shule hiyo, Ndugu ANDREW KAYOLE (32yr), mhitimu wa UDOM, Shahada ya Biashara  Bc(HRM) amesema Shule hiyo ilisajiliwa rasmi tarehe 21.6.2017 na tayari WAHITIMU wa kwanza wamemaliza Darasa la 7 (Std 7) Mwaka jana (2019) wakiwa wa KWANZA kwa Wilaya ya Musoma katika kundi lao. 
Wanafunzi wote walifaulu (A&B). Shule inafundisha kwa lugha ya KIINGEREZA na Mwakani lugha ya KIFARANSA itaanza kufundishwa Shuleni hapo.
MGENI RASMI, Mbunge wa Jimbo la Musoma Vijijini, Prof Sospeter Muhongo amesema kwamba kuwepo kwa Shule Binafsi (Private Schools) Jimboni mwao ni muhimu sana kwa UIMARIKAJI wa UBORA wa ELIMU kupitia USHINDANI KITAALUMA kwa Shule zote za Msingi zilizoko Jimboni humo (Shule 3 za Binafsi na 111 za Serikali).
Mbunge huyo amekuwa AKICHANGIA MAENDELEO ya Shule za Msingi na Sekondari za Serikali na Binafsi bila UBAGUZI wo wote. 
Aliwakumbusha WAGENI waalikwa kwamba Vyuo Vikuu bora Duniani vimo vya Binafsi (Private Universities) kama vile Harvard (USA),  MIT (USA), Yale (USA) Caltech (USA), na vilevile vimo vya umma (Public Universities) kama vile Oxford (UK) na Cambridge (UK).
Mbunge huyo amechangia box 10 za VITABU vya Maktaba ya Shule hiyo. Vilevile, amechangia SARUJI MIFUKO 50 kwa ajili ya ujenzi wa Jengo la TEHAMA. Ametoa ahadi ya kuchangia COMPUTER 1 na PRINTER 1 mara Jengo hilo litakapokamilika na kuanza kutumika.
Wakati akizindua AGAPE Primary School na kuweka Jiwe la Msingi la Jengo la TEHAMA la Shule hiyo, Mbunge huyo AMEMWOMBA MWANZILISHI wa Shule hiyo aendelee kuipanua hadi kuanza kutoa MASOMO ya SEKONDARI.
WAZALIWA KUWEKEZA VIJIJINI MWAO
MMILIKI (Ndugu ANDREW KAYOLE) wa Agape Primary School ni KIJANA (32yr) ALIYETHUBUTU na KUFANIKIWA kuwekeza Kijiji mwao. 
 Mbunge wa Jimbo AMEMPONGEZA SANA na kusema JIMBO LINAJIVUNIA kuwa na WAWEKEZAJI wa aina hiyo – TUJIFUNZE KWAKE na TUWEKEZE Vijijini kwetu!
 MGENI RASMI, Mbunge wa Jimbo la Musoma Vijijini, Prof Sospeter Muhongo (kushoto)  na mmiliki wa shule hiyo,  Andrew Kayole (wa pili kulia) pamoja na viongozi wa mbalimbali wakipiga makofi ikiwa ni ishara ya kufurahia baada ya  kuzindua rasmi shule hiyo.
 Profesa Muhongo akiangalia jiwe la msingi baada ya kuizindua rasmi shule hiyo.
 Profesa Muhongo akiwa na viongozi wengine pamoja baadhi ya wanafunzi wa shule hiyo
 Mbunge wa Jimbo la Musoma Vijijini, Prof. Muhongo (kulia) akizungumza jambo na viongozi pamoja na mmiliki wa shule hiyo, Kayole.
Prof. MUHONGO AKIWA NA BAADHI YA VIONGOZI PAMOJA NA BAADHI YA WANAFUNZI BAADA YA KUZINDUA SHULE HIYO YA AGAPE.



  • Share
  • Tweet
  • Share



    • Email

    Post navigation

    ← HAYUPO MWANAFUNZI WA KIDATO CHA…


    Tafuta katika Tovuti hii

    Machapisho ya Karibuni

    • MZALIWA WA KIJIJI CHA BUKIMA AANZISHA SHULE YA MSINGI KIJIJINI MWAO – YAZINDULIWA RASMI LEO January 8, 2020
    • HAYUPO MWANAFUNZI WA KIDATO CHA KWANZA 2020 (wamechaguliwa 3,502) ATAKAYEBAKI NYUMBANI January 6, 2020
    • MICHEZO JIMBONI – UTEKELEZAJI WA ILANI YA CCM YA 2015-2020 January 1, 2020
    • MASHINDANO YA KUPIGA KASIA 2019 (THE ANNUAL BOAT RACE) December 29, 2019
    • SIKUKUU YA KRISMASI KIJIJINI NYASAUNGU – WANAKIJIJI WASISITIZA SEKONDARI YAO KUFUNGULIWA MWAKANI (2020) December 27, 2019

    Kalenda

    January 2020
    M T W T F S S
    « Dec
    1 2 3 4 5
    6 7 8 9 10 11 12
    13 14 15 16 17 18 19
    20 21 22 23 24 25 26
    27 28 29 30 31
  • email
  • facebook
  • linkedin
  • twitter
  • reddit
  • google+
author

Author Name

Author Description!

Get Free Email Updates to your Inbox!
  • Rss
  • Twitter
  • FaceBook
  • Google +

Post a Comment

« Newer Posts Older Posts »

Popular Posts

  • PICHA: UFUNGUZI WA MAFUNZO YA SIKU MBILI YA MITAALA ILIYOBORESHWA YALIYOANZA LEO KATIKA CHUO CHA UALIMU, MOROGORO
    Naibu katibu Mkuu Wizara ya Elimu Sayansi na Teknolojia Dk. Frankilin Rwezimula, akifungua mafunzo ya Mtaala ulioboreshwa yaliyokuwa mahusu...
  • MSIGWA AELEZA UMUHIMU WAHARIRI WA HABARI, TAASISI ZA UMMA KUKUTANA.
     Na Mwandishi Wetu Dodoma MSEMAJI Mkuu wa Serikali na Mkurugenzi wa Idara ya Habari (MAELEZO) Gerson Msigwa amesema kuna umuhimu wa wahar...
  • DK. MPANGO: WATANZANIA TUOMBE TOBA KWA MUNGU KUFUTA MATENDO YA UKATILI YANAYOKITHIRI DHIDI YA WATOTO
    Dodoma, leo Makamu wa Rais Dk. Philip Mpango, ametoa mwito kwa Watanzania kuomba toba kwa Mungu kwa matendo ya kikatili kwa Watoto na kuach...

www.CodeNirvana.in

Magazeti Ya Leo

Back To Top
Copyright © Magazeti ya Leo, Habari Leo Tanzania, Mwananchi, Michuzi, mwanaspoti, nipashe, Udaku | Designed By Code Nirvana