Mbunge wa Jimbo la Musoma Vijijini, Prof. Sospeter Muhongo amepanga kuongoza harambee ya kuchangia fedha za kujengea vyumba vya madarasa 13 katika shule zenye ufungufu jimboni humo.
Katika harambee hiyo Prof. Muhongo atawashirikisha wanavijiji mbalimbali ili kutimiza lengo la kunusuru hali hiyo itakayookoa wanafunzi 616 wanaotarajia kujiunga Kidato cha Kwanza mwaka huu katika shule hizo zenye upungufu wa vyumva vya madarasa.
Mbunge Muhongo anataajia kutembelea shule zote za sekondari zenye upungufu huo na hatimaye kuandaa harambee ya kuwezesha ujenzi wa vyumba hivyo haraka iwezekanavyo ili wanafunzi wasikose kujiunga.
“Shule zinafunguliwa Jumatatu, tarehe 6.1.2020, bado tunao upungufu wa vyumba 13 vya Madarasa ya Kidato cha Kwanza (Form I).
Vyumba 13 hivyo visipopatikana wanafunzi 616 watabaki nyumbani wakisubiri uwepo wa Vyumba vya Madarasa yao,” alisema Prof. Muhongo hivi karibuni jimboni humo.
.
Ameanza kutembelea shule hizo leo na kuona kila shule vyumba vilivyopungua.
Ratiba kamili ya kukagua shule hizo ni kama ifuatavyo; upungufu wa vyumba kwenye mabano.
Tarehe 2.1.2020
Saa 4 Asubuhi
Busambara Secondary School (Mpya)
Saa 8 Mchana
Bugwema Sekondary School (Vyumba 3)
Tarehe 3.1.2020
Saa 4 Asubuhi
Dan Mapigano Memorial Secondary School (Mpya)
Saa 8 Mchana
Bulinga Secondary School (Vyumba 3)
Tarehe 6.1.2020
Saa 4 Asubuhi
Nyakatende Secondary School (Vyumba 2)
Saa 8 Mchana
Rusoli Secondary School (Chumba 1)
Kasoma Secondary School (Vyumba 3) na Nyanja Secondary School (Chumba 1) BADO WANAJIPANGA
Kwa WANAOPENDA KUCHANGIA ujenzi huo hata kwa kupitia Akaunti za Benki za Sekondari hizo, wanaombwa wapewe mawasiliano ya KUCHANGIA kutoka kwa:
Fedson: 0765 59 28 28
Hamisa: 0762 62 68 81
Verediana: 0764 23 98 21
SISI SOTE tunaombwa TUCHANGIE UJENZI WA VYUMBA 13 vinavyohitajika ili WANAFUNZI 619 wa FORM I wa Jimboni mwetu WASIKOSE kuanza MASOMO yao ya Sekondari.
HERI YA MWAKA MPYA WENYE MAFANIKIO MAKUBWA
TUHAKIKISHE WANAFUNZI WALIOFAULU NA KUCHAGULIWA KUJIUNGA NA FORM I JANUARI 2020 WANAENDA KUANZA MASOMO YAO KWENYE SEKONDARI WALIZOPANGIWA
KIDATO CHA KWANZA 2020 - KIMEPUNGUKIWA VYUMBA VYA MADARASA 13, WANAFUNZI 619 WATABAKI NYUMBANI

Post a Comment