Rais Dk. John Magufuli amemteua George Simbachawene kuwa Waziri wa Mambo ya Ndani kuchukua nafasi ya Kangi Lugola ambaye uteuzi wake umetenguliwa huku Rais akimteua Mbunge wa Ilala Musa Azan Zungu kuwa Waziri wa nchi, Ofisi ya Rais anayeshughulikia Muungano na mazingira., kujaza nafasi iliyoachwa na Simbachawene.
Hatua hiyo imekuja baada ya Rais Magufuli kuonesha kutofurahishwa na utendaji wa wizara hiyo chini ya aliyekuwa waziri wake Kangi Lugola.
Akizungumza katika hafla ya kukabidhi nyumba za askari magereza Ukonga jijini Dar es Salaam, kingozi huyo amesema kuwa licha ya kuwa rafiki mkubwa wa kiongozi huyo, hafai kusalia katika ofisi yake kutokana na makosa aliyoyafanya.
Akionesha kusikitishwa kwake Rais Magufuli alisema: ''Tuna changamoto nyingi na hasa hii ya Mambo ya Ndani, kama kuna wizara inanitesa ni wizara ya mambo ya ndani, nataka muelewe hivyo watanzania, inatesa sana''
''Katika kipindi cha miaka minne kuna tume nyingi tu zimeundwa kwa ajili ya kuchunguza wizara ya mambo ya ndani kwa miradi ya hovyo iliyokuwa ikifanyika, na mimi nilitegemea watu watakuwa wanajifunza''.
Hivi karibuni kulikuwa na mkataba mmoja wa ajabu unatengenezwa wizara ya mambo ya ndani wenye thamani ya Euro milioni 408 , mradi huo umetayarishwa na kusainiwa na Kamishna Jenrali wa zimamoto, haujapangwa kwenye bajeti wala kupitishwa na Bunge. ''
Post a Comment