Featured

    Featured Posts

RAIS WA ZANZIBAR DK.SHEIN AWEKA JIWE LA MSINGI JENGO LA MICHEZANI MALL NA LA SHEIKH THABIT KOMBO MICHEZANI IKIWA NI SHAMRA SHAMRA ZA MIAKA 56 YA MAPINDUZI YA ZANZIBAR.

 RAIS wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Mhe.Dk. Ali Mohamed Shein, akiondoa kipazia kuashiria kuweka jiwe la Msingi la Jengo la Michezani Mall Jijini Zanzibar, (kushoto kwa Rais) Waziri wa Fedha na Mipango Zanzibar.Mhe.Mohammed Ramia Abdiwawa, hafla hiyo imefanyika katika viwanja vya michezani Jijini Zanzibar ikiwa ni shamrashamra za kuadhimisha Miaka 56 ya Mapinduzi ya Zanzibar.(Picha na Ikulu)
RAIS wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Mhe.Dk.Ali Mohamed Shein akiwa na Waziri wa Fedha na Mipango Zanzibar.Mhe.Balozi Mohammed Ramia Abdiwawa na Mkuu wa Mkoa wa Mjini Magharibi Unguja.Mhe.Hassan Khatib Hassan (kulia kwa Rais) na (kushoto kwa Rais) Naibu Katibu Mkuu wa CCM Zanzibar.Dr. Abdalla Juma Mabodi, wakielekea katika jengo la Sheikh Thabit Kombo kwa aajili ya uwekaji wa Jiwe la Msingi la Jengo hilo ikiwa ni shamrashamra za kusherehekea Miaka 56 ya Mapinduzi ya Zanzibar.(Picha na Ikulu)  
RAIS wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baeraza la Mapinduzi Mhe.Dk. Ali Mohamed Shein akisalimiana na Waziri wa Fedha na Mipango Zanzibar.Mhe.Balozi Mohammed Ramia Abdiwawa, alipowasili katika viwanja vya Mradi wa Ujenzi wa Maduka ya Kisasa Michezani Mall na Jengo la Sheikh Thabit Kombo  wakati wa hafla ya uwekaji wa Jiwe la Msingi la jengo hilo linalojengwa na Kampuni kutoka China ya CRJE, ikiwa ni shamrashamra za kusherehekea Miaka 56 ya Mapinduzi ya Zanzibar.(Picha na Ikulu).
RAIS wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Mhe.Dk. Ali Mohamed Shein, akisalimiana na Viongozi wa Kampuni ya Ujenzi ya CRJE kutoka Nchini China, aliposiki katika viwanja vya Michezani Mall, kwa ajili ya Uwekaji wa Jiwe la Msingi la jengo hilo, ikiwa ni shamrashara za Miaka 56 ya Mapinduzi ya Zanzibar.(Picha na Ikulu)
RAIS wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Mhe.Dk. Ali Mohamed Shein akimsikiliza Meneja wa Mipango, Uwekezaji na Utafiti wa Mfuko wa Hifadhi ya Jamii Zanzibar.(ZSSF) Ndg. Abdulazizi Ibrahim Iddi akitowa maselezo ya michoro ya picha ya jengo la Michezani Mall, wakati wa hafla ya Uwekaji wa Jiwe la Msingi,ikiwa ni shamrashamra za kusherehekea Miaka 56 ya Mapinduzi ya Zanzibar na  (kushoto kwa Rais) Waziri wa Fedha na Mipango Zanzibar.Mhe Balozi Mohammed Ramia Abdiwawa, hafla hiyo imefanyika katika viwanja vya jengo hilo michezani Jijini Zanzibar.(Picha na Ikulu)
author

Author Name

Author Description!

Get Free Email Updates to your Inbox!

Post a Comment

www.CodeNirvana.in

Magazeti Ya Leo

Copyright © Magazeti ya Leo, Habari Leo Tanzania, Mwananchi, Michuzi, mwanaspoti, nipashe, Udaku | Designed By Code Nirvana