Shughuli maalumu ya maombolezo ya kuuaga mwili wa shahidi Qassem Soleimani, kamanda wa kikosi cha Quds cha Jeshi la Walinzi wa Mapinduzi ya Kiislamu (IRGC) pamoja na wanamapambano wenzake waliouawa shahidi pamoja naye imefanyika katika mji wa Kadhimain nchini Iraq.
Shughuli ya kuuaga mwili wa shahidi Qassem Soleimani, kamanda wa kikosi cha Quds cha Jeshi la Walinzi wa Mapinduzi ya Kiislamu (IRGC), Abu Mahdi al Muhandis, Naibu Mkuu wa Harakati ya Kujitolea ya Wananchi wa Iraq (Al Hashd al Shaabi) pamoja na wanamapambano wengine waliouawa shahidi pamoja nao imefanyika mapema leo mjini Kadhimain kwa kuhudhuriwa na umati mkubwa wa wananchi wa Iraq.
Kutokana na ombi la wananchi wa Iraq, viwiliwili vya mashahidi hao wa shambulio la kigaidi la usiku wa kuamkia Ijumaa lililofanywa na majeshi vamizi na ya kigaidi ya Marekani karibu na uwanja wa ndege wa Baghdad, vitaagwa na kusindikizwa pia katika miji ya Najaf na Karbala.
Kwa mujibu wa tangazo la ofisi ya kamandi kuu ya kikosi cha Quds cha IRGC, watu 10 waliuliwa shahidi katika shambulio hilo la kigaidi lililofanywa na Marekani, ambapo watano miongoni mwao akiwemo Luteni Jenerali Qassem Soleimani ni Wairani na mashahidi watano wengine akiwemo Abu Mahdi la Muhandis, ni Wairaqi.
Viwiliwili vya mashahidi wa Iran itasafirishwa kuletwa hapa Tehran leo jioni.../
Post a Comment