Na Lydia Lugakila:-Kagera
Watu watano katika kata ya Bugomora wilayani Kyerwa mkoani Kagera wameripotiwa kung'atwa na mbwa wenye kichaa.
Kauli hiyo imetolewa na Diwani wa kata ya Bugomora Tulakila Twijuke wakati akizungumza na viongozi mbali mbali wa kata hiyo pamoja na wananchi juu ya tukio la kuzuka kwa kichaa cha mbwa ambacho tayari mpaka sasa kimeleta madhara ya kung'atwa kwa watu watano.
Tulakila amesema kuwa tangu tukio hilo limeisharipotiwa panapohusika na tatizo lililopo ni ukosefu wa chanjo ya kichaa cha mbwa licha ya kwamba wanaong'atwa wanapatiwa chanjo.
Kutokana na hali hiyo Diwani huyo amewataka wafugaji wa mbwa katani humo kufungua mbwa wote hao mapema saa kumi na mbili jioni hadi saa nne usiku ili kukwepa madhara hayo na kutokwamisha shughuli za wananchi hao.
Amesema awali taarifa hizo zilimfikia Daktari wa mifugo wilayani Kyerwa Prosper Rutakinikwa na kuahidi kulitatua tatizo kwa kufuatilia chanjo ya kichaa cha mbwa mkoani Mwanza.
Diwani Twijuke ameongeza kuwa tayari hatua zimechukuliwa ikiwemo wananchi katani humo kutangaziwa kuhusu kufunga mbwa hao, na kuwafungua usiku huku wakihimizwa kuweka matangazo yanayotambulisha sehemu zote ambazo zina mbwa wenye kichaa.
Hata hivyo Diwani huyo amesema hakuna vifo vitokanavyo na madhara hayo na kukitaja kituo cha Nkwenda na Kaisho kutumika katika kuwahudumia wananchi waliong'atwa na mbwa hao.
Author Name
Author Description!
Get Free Email Updates to your Inbox!
Post a Comment