Featured

    Featured Posts

WAUAWA ZAIDI YA WANAHARAKATI 550 KATIKA KIPINDI CHA MIAKA MINNE ILIYOPITA

  • Jumla ya wanaharakati wa kijamii 555 nchini Colombia wameuawa katika kipindi cha miaka minne iliyopita.
Idara ya mwanasheria wa umma ambayo inajishughulisha na kutetea haki za kiraia nchini Colombia imetangaza kwamba, kati ya mwaka 2016 na 2019 kwa akali wanaharakati wa kijamii wapatao 555 ambao walikuwa wakijishughulisha kutetea haki za wananchi, wameuawa nchini humo. Carlos Negret, mwanasheria wa umma nchini Colombia amesema kuwa mauaji dhidi ya viongozi hao wa kijamii ambao waliyatoa muhanga maisha yao kwa ajili ya kutetea usawa wa kijamii nchini, yameutia doa uga wa haki za binaadamu na demokrasia ndani ya Colombia.
Mauaji nchini Colombia
Kadhalika Carlos Negret ameonyesha wasi wasi wake wa kutokuwepo irada ya kisiasa yenye lengo la kuzuia hatua hizo na kuwatetea viongozi hao wa kijamii nchini humo na badala yake watu ambao wanafanya juhudi za kupigania usalama na amani ya nchi ndio wamekuwa wakiuawa. Mwanasheria huyo wa umma wa Colombia amesisitiza kwamba viongozi wa serikali ni lazima wafanye haraka kuandaa mazingira ya lazima kwa ajili ya kutatua tatizo hilo. HIi ni katika hali ambayo kwa mara kadhaa asasi mbalimbali za kimataifa likiwemo Shirika la Kutetea Haki za Binaadamu pia zimewahi kuitaka serika ya Bogota kuzuia mauaji dhidi ya wanaharakati hao wa kijamii nchini humo.
author

Author Name

Author Description!

Get Free Email Updates to your Inbox!

Post a Comment

www.CodeNirvana.in

Magazeti Ya Leo

Copyright © Magazeti ya Leo, Habari Leo Tanzania, Mwananchi, Michuzi, mwanaspoti, nipashe, Udaku | Designed By Code Nirvana