Mbali na kuondolewa katika mashindano Klabu ya yanga inatoa shukrani kwa serikali ya Mapinduzi Zanzibar na waandaaji wa kombe la mapinduzi kwa kuipa nafasi timu yao kwa kushiriki michuano hiyo muhimu na ya Kihistoria.
Imesema inathamini na kutambua michuano hiyo na timu yao ilidhamilia kutwaa taji hilo ila baati mbaya imetokea timu imeondolewa kwa mikwaju ya penati.
"Yanga kama klabu tunayaheshimu mashindano hayo kutokana yanatukutanisha kama Taifa na kutoa tafsiri ya muungano wetu hasa kwenye mchezo wa mpira wa miguu hivyo tutaendelea kushiriki michuano hiyo katika miaka ijayo"
Post a Comment