Mratibu wa Huduma za Maabara Wilaya ya Kigamboni, Grace Maliva, akizungumza waandishi wa habari hawapo pichani mara. (PICHA NA KHAMISI MUSSA)
Na Asha Mwakyonde
MRATIBU wa Huduma za Maabara Wilaya ya Kigamboni, Grace Maliva amemshukuru Rais John Magufuli kwa kuwezesha kupatikana Maabara kubwa tatu za kisasa katika wilaya hiyo kwa kipindi kifupi tangu mchakato wa ujenzi ulivyoanza.
Haya ameyasema jijini Dar es Salaam Februari 11, 2020 mara baada ya Magufuli kuzindua Wilaya mpya ya Kigamboni pamoja na majengo ya maabara, Grace amesema serikali ya awamu ya tano imeweka kipaumbele cha kujali afya za Watanzania ambao ndio walipata kodi.
Mratibu huyo amesema upatikanaji wa maabara hizo zitarahisisha kupunguza msongamano wa wagonjwa wanaohitaji vipimo na kwamba watahudumiwa kwa wakati pindi zitakapokamilika tofauti na hali ilivyo sasa.
Ameongeza kuwa awali hali ilikuwa mbaya kwani wilaya nzima yenye kata 67 ilikuwa na Maabara moja ambayo ni vijibweni na vyumba vilivyokuwa mfano wa Maabara vitatu.
Amefafanua kwamba maabara moja ipo katika kituo cha afya Kimbiji, kingine kituo cha afya cha Kigamboni na kwamba kimoja kipo Somagila Mjimwema ambapo ndio hospital ya wilaya.
"Mafanikio haya yanatokana jitihada zinazofanywa na Waziri wa Afya, Maendeleo ya Jamii, Jinsia, Wazee na Watoto Ummy Mwalimu kwa kuhakikisha huduma za afya zinaboreshwa na hii ni pamoja na ujenzi wa maabara, kama hizi na vifaa," amesema Grace.
Aidha amemshukuru Rais Magufuli kwa kujali watumiaji wa majengo husika na kuwaweka kwenye kamati za ujenzi na kuwa washauri wa karibu wa miundombinu inayojengwa hasa upande wa Maabara.
Post a Comment