Featured

    Featured Posts

ATOA MAAGIZO KWA WENYEVITI WA VIJIJI NA VITONGOJI

 Mwenyekiti wa chama cha mapinduzi CCM Wilayani Muleba mkoani Kagera Athuman Kahara akizungumza na wananchi katika sherehe hizo

 Diwani wa kata ya Mushabago Mh Aron Mpumbya akipongeza serikali juu ya miradi inayoendelea kutekelezwa
 Ukaguzi wa mradi wa ujenzi wa shule ya Sekondari Nyakatanga
 Sehemu ya wanachama walioudhulia sherehe hizo
Mwenyekiti Wa chama cha mapinduzi CCM Wilayani Muleba Athuman Kahara akifungulia maji katika mradi huo

Na Lydia Lugakila Kagera:-

Mwenyekiti wa chama cha Mapinduzi CCM wilayani Muleba mkoani Kagera Athuman Kahara ametoa agizo kwa wenyeviti wa vijiji na vitongoji walioteuliwa na chama cha mapinduzi katika nafasi zao kuhakikisha wanaunda mtandao mkubwa wa kusikiliza kero za wananchi mara moja hasa walioko katika makundi maalum wakiwamo wazee huku akiahidi kufukuzwa chama watendaji watakaoshindwa kutekeleza agizo hilo.

Kauli hiyo imetolewa na mwenyekiti wa chama cha mapinduzi CCM wilayani Muleba mkoani Kagera Athuman Kahara wakati akihitimisha maadhimisho ya miaka 43 ya kuzaliwa kwa chama hicho yaliyofanyika katika shule ya msingi Mwijage iliyopo katika kata ya Mushabago wilayani Muleba.

Athumani Kahara amesema kuna baadhi ya makundi maalum bado yananyanyasika katika jamii huku akitaja kundi la wazee ambalo muda mwingi ubugudhiwa hasa kusukumwa na vijana pale wanapokuwa katika harakati za kufuata huduma mbali mbali hasa za  matibabu ambapo hufanyiwa vurugu na vijana kwa kuambiwa muda wao wa kuishi umeisha jambo ambalo amelitaja kama kero na kuagiza watendaji hao kuunda mtandao wa kushughulikia kero za makundi  Mara moja na kuwa watakaoshindwa watabakia kusema nilikuaga CCM.

Mwenyekiti huyo amesema kuwa hakuna sababu ya kudharau makundi maalum kwani nayo yanastahili haki sawa na kutaja kundi la wazee kuhusika pakubwa kulitetea taifa hili kutoka katika ukoloni.

"Natamka siko au chama hakiko tayari kuona wazee wananyanyaswa enyi watendaji shughulikieni kero hizo Mara moja na tambua wazee wapo, walikuwepo na wataendelea kuwepo hivyo mtendaji lege lege hatumuwezi katika chama hiki" alisema Kahara.

Mwenyekiti huyo amesema kuwa wazee hao wanapaswa kupewa heshima zote kwani wamehusika pakubwa hasa kuwaandaa vijana ambao mpaka sasa ni viongozi imara.

Amewahimiza watendaji  hao wa serikali kushughulikia vijana wanaowabugudhi wazee kwa kuwasukuma hasa pale wanapokuwa wakifuata huduma ya matibabu kwani kufanya hivyo ni dhambi kubwa badala yake wawaheshimu, wawajali na kuwapenda pia kuwasaidia kazi ngumu.

Ameongeza kuwa wazee wametenda mambo mengi hivyo  watendaji wa serikali wahakikishe wazee hao wanapata huduma stahiki bila kujali kabila, itikadi za vyama vyao wala dini.

Sherehe hizo zimeambatana na matukio mbali mbali ikiwemo kutembelea mradi wa maji Rushwa na Bulyage, ujenzi wa sekondari Nyakatanga pamoja na zoezi kubwa la ugawaji vitambulisho vya matibabu ya wazee 

Kwa upande wake diwani wa kata ya Mushabago Mh.Aron Mpumbya ameishukuru serikali ya Jamhuli ya Muungano wa Tanzania inayoongozwa na Rais John Pombe Magufuli kwa kujitoa pakubwa kuwahudumia wananchi katika miradi mbali mbali ya kimaendeleo ambayo imekamilika kwa kiwango kikubwa.

Mh. Mpumbya ameahidi kuendelea kuhimiza jamii hasa katika shughuli za kimaendeleo.

Maadhimisho hayo ya kuzaliwa kwa chama cha mapinduzi CCM ki mkoa yamefanyika wilayani Ngara mkoani Kagera huku kiwilaya yamefanyika katika kata ya Mushabago wilayani Muleba na kubeba kauli mbiu isemayo miaka 43 ya kuzaliwa kwa CCM tumeahidi, Tumetekeleza, na tunaahidi tena kuchapa kazi kwa juhudi, Ubunifu na maarifa Zaidi.
author

Author Name

Author Description!

Get Free Email Updates to your Inbox!

Post a Comment

www.CodeNirvana.in

Magazeti Ya Leo

Copyright © Magazeti ya Leo, Habari Leo Tanzania, Mwananchi, Michuzi, mwanaspoti, nipashe, Udaku | Designed By Code Nirvana