Kamati ya siasa ya Chama Cha Mapinuzi (CCM) Wilayani Kibondo mkoani Kigoma imemtaka Mkuu wa Wilaya Kibondo kufuatilia kwa kina waliohujumu mradi wa maji uliopo katika kijiji cha Minyinya wilayani hapa, uligharimu kiasi cha sh. Milioni 700,500,000 .
Akiwakilisha taarifa ya mradi huo mbele ya Kamati ya Siasa ya CCM, Michael Marcelo kwa niaba ya Meneja wa Mamlaka ya Maji Mjini na vijijini RUWASA amesema mradi huo ulianza tarehe 1/12/2012 na kukamilika 1/5/2013 na kwamba ujenzi huo wa mradi ulijumuisha ujenzi uliofanyika katika kijiji cha Nyagwijima Kakonko katika mkataba mmoja.
Kwa upande wake Mwenyekiti wa CCM wilaya ya Kibondo Hamis Tahilo hakuridhishwa na taarifa hiyo ya mradi wa maji alihitaji mashine iwashwe ili ianze kuvuta maji ndipo mhudumu wa mashine ya kusukuma maji akasema mashine haiwezi kuwaka sababu haina betri kauli iliyoleta utata.
Nae Katibu wa CCM Wilayani Kibondo Stainley Mkandawile alisema kutokana na taarifa iliyo somwa inaonesha dhahili kuwa kuna uhujumu uliofanyika katika mrai huo hivyo ofisi ya Mkuu wa Wilaya haina budi kufuatilia hujuma iliyofanyika na walio husika hatua kali zichukuliwe dhidi yao.
Hirida Noberth ambae ni mkazi wa kijiji cha Minyinya alisema tangu mradi huo ukamilike ujenzi wake kijiji cha Minyinya hakijapata maji yatokanayo na mradi huo kwani wananchi wa kijiji hicho wanatembea umbali mrefu sana kutafuta maji kitendo kinachowafanya kukosa mda wa kufanya shughuli za kuwaigizia kipato.
Post a Comment