Aliyekuwa Diwani wa Kata ya Kagera katika Manispaa ya Kigoma-Ujiji kwa tiketi ya chama cha ACT-Wazalendo kinachoongozwa na Zitto Kabwe, Ismail Mahamudu akizungumza mbele ya waandishi wa habari, baada ya yeye na madiwani wengine wanne wa chama hicho, kutangaza kung'oka ACT-Wazalendo.na kujiunga na Chama Cha Mapinduzi (CCM), katika mkutano na waandishi hao uliofanyika leo katika Ofisi Ndogo ya Makao Makuu ya CCM, Lumumba jijini Dar es Salaam. Kulia ni Katibu Mkuu wa CCM Dk. Bashiru Ally na Katibu wa NEC, Itikadi na Uenezi Humphrey Polepole wakimsikiliza kwa makini Diwani huyo. Picha: Bashir Nkoromo
Na Bashir Nkoromo, Dar es Salaam
CHAMA Cha ACT-Wazalendo kinachoongozwa na Zitto Kabwe kimepata maafa kufuatia kukimbiwa na madiwani wake watano kutoka Manispaa ya Kigoma-Ujiji, kukikimbia chama hicho na kujiunga na Chama Cha Mapinduzi (CCM).
Madiwani hao ni Musa Jumanne Ngogolwa ambaye alikuwa Diwani wa Kata ya Kipampa, Hamdun Nassoro aliyekuwa Diwani wa Kata ya Kasingirima, Khamis Rashid Khamis aliyekuwa Diwani Kata ya Gungu, Fuadi Seif Nassoro aliyekuwa Diwani Kata ya Kasimbu na Ismail Mahamudu aliyekuwa Diwani wa Kata ya Kagera.
Wakizungumza kwa nyakati tofauti mbele ya Katibu Mkuu wa CCM Dk. Bashiru Ally ambaye amewapokea katika Ofisi Ndogo ya Makao makuu ya CCM Lumumba jijini Dar es Salaam, leo wamesema wameamua kung'oka ACT-Wazalendo na kujiunga na CCM bada ya kuridhishwa na utendaji kazi mzuri wa Mwenyekiti wa CCM, Rais Dk. Magufuli.
"Ni kichaa tu ndiyo anaweza kutokubali kwamba Rais Dk. Magufuli anafanya kazi nzuri na kubwa kwa ajili ya kuiboresha Tanania na watu wake, hivyo mimi binafsi bila shaka hata na wenzangu tumeamua kuja CCM ili tumuunge mkono Rais huyu kwa uhuru mpana zaidi", alisema mmoja wa madiwani hao Khamis Rashid Khamis.
"Sisi lengo letu lililotufanya kufanya kazi ya siasa kwenye Chama cha Upinzani cha ACT-Maendeleo ilikuwa ni kutaka kuchangia mawazo yetu katika kuijenga Tanzania, lakini sasa tumebaini kuwa chama hiki hasa kiongozi wake bwana Zitto Kabwe hana nia ya kujenga nchi bali kubomoa" alisema Diwani mwingine Fuadi Seif Nassoro.
Post a Comment